Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amekagua Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kimagai iliyopo Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma,ambao mpaka sasa ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 14 ambazo zimetokana na Michango mbalimbali ya Wananchi pamoja na Nguvu kazi.
Kwa
Mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
amesema lengo la Mradi huo ni Kupunguza Changamoto ya Upatikanaji wa
Huduma za Afya kwa Wananchi kwenye Kijiji hicho.
Akiwa kwenye
ziara hiyo Juni 15,2023 Wilayani humo,baada ya kukagua ujenzi wa
Zahanati, Katibu Mkuu Chongolo akachangia Mifuko 50 ya Saruji ili
kuharakisha Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya na Kusogeza Huduma karibu kwa
Wananchi.
"Kwenye Sekta ya Afya kazi kubwa inafanyika, Serikali
inafanya hivyo Sababu inao wajibu wa kumlinda kila raia wa nchi hii ili
kuongeza nguvu kazi, lakini kwenye vituo vya Afya kulikuwa na Changamoto
ya Vifaa tiba,
lakini tumezungumza na Wahusika Tamisemi, Wizara
ya Afya Kupitia MSD kwamba ifikapo mwezi wa Nane hili zoezi la Vifaa
tiba liwe limefikia Ukomo wake ili Wananchi waanze kunufaika na Vifaa
tiba vilivyoletwa kwenye Vituo vyote vya Afya nchi nzima" amesema
Chongolo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo wa CCM Daniel
Chongolo ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema
pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu.


Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kimagai wakifurahia ujio wa Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo katika eneo hilo la ujenzi wa Zahanati yao
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kimagai wakifurahia ujio wa Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo katika eneo hilo la ujenzi wa Zahanati yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...