Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MAMLAKA ya Masoko na Mitaji (CMSA) kwa kushirikiana na SIDO leo Juni 22 mwaka 2023 wameendesha warsha ya kuwajengea uwezo na uelewa wadau ambao ni wajasiriamali kuhusu mpango wa kuwezesha kupatikana fedha kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo na za kati (Mitaji Halaiki).

Akizungumza Juni 22, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa semina hiyo Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na Mipango katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Alfred Mkombo amesema lengo ni kuwajengea uwezo na uelewa wadau wakiwemo wanyabiashara ndogo ndogo na kati pamoja na wajasiriamali kuhusu mitaji halaiki.

"Mitaji Halaiki ni mpango wa kuwezesha kupatikana kwa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo na za kati kutoka kwenye makundi na mitaji hlaiki, kimsingi ni matumizi ya mitandao platfom maana yake unatumia electronic platfom kukusanya fedha kwa ajili ya wawekezaji kuendesha biashara zao.

" Na sasa hivi Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kwa kushirikiana na wadau tumeandaa miongozo hii itakayosimamia uendeshaji wa majukumu ya majukwaa ya mitaji halaiki.


"Majukwaa haya yanatajwa kwamba yatawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kuweka mawazo yao katika majukwaa ya haya na kupata wawekezaji na kuendesha biashara zao, "amesema.

Akifafanua zaidi anasema katika semina hiyo wameshirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo SIDO, Tanzania Setup Assocition , COSTECH pamoja na wafanyabiashara ambao wanatarajia kuendesha majukwaa hayo.

Amesema wajasiriamali ambao wanatarajia kutumia majukwaa hayo ni wajasiriamali ambao tayari wameshasajili biashara zao na zinajukulikana." Tutaanza kwa kutoa leseni kwa waendeshaji wa majukwaa baada ya kutoa leseni hayo majukwaa ndio yatatumika kwa wafanyabiashara kutuma taarifa za biashara zao ili kupata hizo fedha.


"Kwa hiyo ni wafanyabiashara wale wadogo na wakati na kwasababu ni biashara zinazoanza , hata hivyo kutakuwa na ukomo ambao muwekezaji hata ruhusiwa kuvuka kwasababu asije akapoteza fedha zake ikitokea tatizo lolote lakini haya majukwaa yatasimamiwa na hata wafundishaji wa hayo majukwaa watakuwa wanasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, " amesema Mkombo.

Kwa upande wake Mkindo Forogo anayejishughulisha na taka rejea kwa kukusanya chupa za glasi zilizotumika Dar es Salaam na Tanzania nzima amesema warsha hiyo ni muhimu kwao kutokana manufaa waliyoyapata.

"Kwasababu kuna sekta nyingine za kibiashara zilizosahaulika lakini kadri tunavyosogea kwenye warsha kama hizi tunaonekana wanatufahamu, tunazo changamoto nyingi sana za mikopo kwa mabenki mengine madogo madogo ambayo hayatujui japo tunauzoefu wa biashara siku nyingi .

Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na Mipango katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Alfred Mkombo akieleza namna walivyojipanga kuwajengea uwezo na uelewa wadau ambao ni wajasiriamali kuhusu mpango wa kuwezesha kupatikana fedha kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo na za kati (Mitaji Halaiki).
 Mshauri Mkuu wa Ushirikiano, ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,
Cedric Merel akieleza namna wanavyoshiriki kuwawezesha wajasiriamali kuhusu mpango wa kuwezesha kupatikana fedha kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo na za kati (Mitaji Halaiki).

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...