Na Andrew Chale,

TAMASHA la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) linaloendelea visiwani hapa, limeendelea kupambwa na shamra shamra mbalimbali ikiwemo mbio za Ngalawa (Dhow race) ambazo ni miongoni mwa michezo ya asili visiwani hapa inayopendwa na watu wengi toka zamani.

Katika mbio hizo, Ngalawa zaidi 12 ziliweza kushindana kuwania ushindi maalum wa kiasi cha fedha ambapo washiriki uzunguka na Ngalawa hizo bahari ya Hindi.

Akizungumza katika mashindano hayo, Mratibu wa Jukwaa la Wanawake na Vijijini la ZIFF, Sabrina Faraja amesema kuwa washiriki wa Ngalawa hizo hutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar ambapo ufika kushindana na kuwania zawadi zinazotolewa kila mwaka na ZIFF.

"Mshindi wa kwanza anakabidhiwa kitita cha fedha, wa kwanza anapata Laki Saba, na wa Pili Laki Tano huku wa Tatu akipata Laki tatu.

Wengine wanapata kifuta jasho kwa ushiriki wao, huku pia zawadi mbalimbali za ushiriki hutolewa.

Aidha, katika mbio hizo, Ngalawa 12 zilizoahindana, Ngalawa moja ilishindwa kuendelea baada ya kupoteza muelekeo wakati wa kuanza kwa mbio hizo na kufanya Ngalawa 11 pekee kumaliza mbio hizo licha ya kuwa na upepo wa wastani baharini.

Ngalawa zilizoshinda ni pamoja na Ngalawa ya Robin Batista nafasi ya kwanza, nafasi ya pili Ngalawa ya WIOMSA na nafasi ya tatu Ngalawa ya AZAM TV.

Ngalawa zingine ni pamoja na MOZET, kamisheni ya utalii Zanzibar na zingine.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...