Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Erica Yegella aliyehamishiwa Halmashauri ya Mji wa Masasi, amemkabishi rasmi ofisi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Tatu Said Issike.
Makabidhiano hayo yamefanyika Juni 16, 2023 katika ofizi zilizopo Makao makuu ya Wilaya hiyo Mkunwa.
Erica Yegella amemweleza Mkurugenzi Tatu Issike kuwa timu ya wakuu wa Idara na vitengo ya Halmashauri hiyo ina watumishi wenye upendo na wachapa kazi hivyo kamhakikishia kuwa atarajie kufanya kazi katika mazingira ya upendo mkubwa.
Amezitaja fursa zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo kuwa ni pamoja na Kilimo cha Korosho, Nazi, Nyanya, Mpunga, Kunde na mazao mengine kwa upande wa Nchi kavu.
Kwa upande wa Bahari amesema kuna fursa kubwa za uchumi wa Bahari ikiwemo ushuru utokanao na mazao ya Samaki na hivi karibuni walienda Zanzibar kwa ajili ya kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili ifike Mtwara DC kwa ajili mashirikiano ya vyombo vya kisasa vya Uvuvi ili wavuvi waweze kufika katika Bahari kuu.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Tatu Said Issike, amemshukuru Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na amewashukuru watumishi kwa kumpokea pamoja na miongozo ya mtangulizi wake Erica Yegella.
Amesema ili kufikia mafanikio makubwa zaidi ni vema kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano bila kumsahau Mungu.
Amewasihi watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo, Kanuni na sheria ili kufikia kuwa katika Tatu Bora au nambari Wani kwa makusanyo katika nchi ili kuvuka zaidi malengo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...