Tarehe 23 Juni 2023, Serikali ilishuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wawekezaji kwa lengo la kukabiliana na uhaba wa bidhaa muhimu nchini.
Baada ya kukamilika, mradi huo utakaogharimu dola za Kimarekani 238.5 milioni, utaleta ajira mpya zipatazo1404 za moja kwa moja na 15,000 ambazo si za moja kwa moja. Baada ya upanuzi, Kampuni itakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 271,000 za sukari na hivyo kupunguza mahitaji ya uagizwaji sukari kutoka nje.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Guy Williams, wakibadilishana mkataba waliosaini kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...