*Wateja wa Airtel kupata punguzo la papopapo la asilimia 10 kwenye tiketi za ndege
*Tiketi za Flydubai kulipiwa kupitia Airtel Money
Airtel money leo imetangaza ushirika wake na Flydubai, ambapo wateja waliounganishwa na Airtel Money wanaonunua tiketi za Flydubai watapata upendeleo wa punguzo la papopapo la asilimia 10. Promosheni hiyo inayoitwa KWEA PIPA, itawahakikishia watumiaji wa Airtel Money nchi nzima punguzo la asilia 10 litakatwa moja kwa moja kwenye bei ya tiketi za safari moja na zile za kwenda-na-kurudi duniani kila walipiapo tiketi zao kwa kutumia Airtel Money.
Flydubai ni kampuni ya usafirishaji ya gharama nafuu ya Dubai Aviation Corporation inayomilikiwa na serikali ya Falme za Kiarabu ikiwa na makao yake makuu kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Dubai na ambapo inaratibia shughuli zake za usafirishaji.
Akiongea kuhusu ushirika huo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba alisema : ‘ Ushirika wetu na Flydubai unaashiria hatua muhimu kwenye adhma yetu ya kuleta mapinduzi kwenye malipo ya kidijitali na kuyarahisisha kwa faida ya wateja wetu na wafanyabiashara kupitia namba ya Lipa ya Airtel Money.”
“ Tunawapa wateja wetu wa Airtel Money fursa ya kuwa na fikra mpya ya kujichagulia huduma maishani, huku wakiunganishwa na wanafamilia na marafiki , wakati huohuo tukiwapa wafanyabiashara fursa rafiki za kuratibu malipo. Mfumo wa malipo wa Airtel Money umesheheni njia anuwai za malipo zisizo na dosari na zilizo salama na kuwahakikishia wateja wetu mfumo rafiki wenye gharama nafuu. Tunajisikia fahari kuanzisha ushirika na Flydubai ili kupanua wigo wa huduma kwa wateja wetu.”
Promosheni ya KWEA PIPA itarindima kwa muda wa miezi mitatu (3) kuanzia Juni hadi Septemba, ikilenga kutoa huduma kwa wateja wa sasa na watarajiao kujiunga na mtandao wetu.Rugamba aliwaomba wateja kuchangamkia fursa hii, na kuongeza: ‘ Nawaalika wateja wetu tunaowathamini kujinufaisha na KWEA PIPA na kufurahia punguzo la asilimia 10, ili waokoe pesa na muda kupitia mfumo wetu rahisi wa malipo.”
Mbali na punguzo la Flydubai, wateja wa Airtel Money watakaojiunga na promosheni hii vilevile watajitengea nafasi ya kujishinda zawadi za papopapo zitolewazo kupitia promosheni inayoendelea hivi sasa ya UPIGE MWINGI. Promosheni hii imesheheni zawadi lukuki ambazo ni muda wa nyongeza wa maongezi, pikipiki, luninga za kisasa, majokofu na pesa taslimu kuanzi tsh milioni 1 hadi donge nono la tsh milioni 50.
" Airtel Money imeunganishwa na Flydubai, ikiwezesha wateja wetu kununua tiketi moja kwa moja kupitia Airtel Money. Ili kujiunga mteja anatakiwa kubofya *150*60# na kuchagua kipengele cha malipo, au kutumia Airtel Money app. Punde akamilishapo mchakato wa malipo, mteja papopapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kukamilika kwa malipo na tiketi ya kielektroniki itakayotumika kwenye safari yake.
Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Tanzania wa Flydubai Bw. Barani Peters alisema: “ Flydubai inayo furaha kubwa kuingia kwenye ushirika huu wa kipekee na Airtel uliosanifiwa kwa ajili ya wateja wa Flydubai kufaidi punguzo la papopapo la asilimia 10 na kusafiri kwenda wanakohitaji. Promosheni ya KWEA PIPA itatuwezesha kuhudumia wateja wengi zaidi kwa njia ya kidijitali na Airtel Money kwa kuwa ni njia inayofaa na inayoweza kutumiwa mahali popote wakati wowote na hivyo kuhakikisha upatikanani wa usafiri wa uhakika.
Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano ( katikati) akionyesha mfano wa ndege za Flydubai wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Kwea Pipa kwenda Dubai itakayowawezesha wasafiri kupata punguzo la bei la asilimia 10 wanapolipia tiketi za Flydubai kupitia Airtel money . Kutoka kushoto ni Meneja Biashara Mkazi wa Flydubai, Peters Barani na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano ( katikati ), Meneja Biashara Mkazi wa Flydubai, Peters Barani (kushoto) na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Lugamba wakizindua promosheni ya Kwea Pipa kwenda Dubai itakayowawezesha wasafiri kupata punguzo la bei la asilimia 10 wanapolipia tiketi za Flydubai kupitia Airtel money . Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano ( katikati)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa
uzinduzi wa promosheni iitwayo Kwea Pipa kwenda Dubai itakayowawezesha
wasafiri kupata punguzo la bei la asilimia 10 wanapolipia tiketi za
Flydubai kupitia Airtel money . Kushoto ni Meneja Biashara Mkazi wa
Flydubai, Peters Barani na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba.
Mkurugenzi
wa Airtel Money, Andrew Rugamba ( kulia) akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa promosheni iitwayo
Kwea Pipa kwenda Dubai itakayowawezesha wasafiri
kupata punguzo la bei la asilimia 10 wanapolipia tiketi za Flydubai
kupitia Airtel money . Kutoka kushoto ni Meneja Biashara Mkazi wa
Flydubai, Peters Barani na Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano.
Meneja Biashara Mkazi wa Flydubai, Peters Barani (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa promosheni iitwayo Kwea Pipa kwenda Dubai itakayowawezesha wasafiri kupata punguzo la bei la asilimia 10 wanapolipia tiketi za Flydubai kupitia Airtel money . Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...