Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Alhamisi, Juni 21, 2023 amepokea taarifa ya
Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa
mapendekezo ya kutatua changamoto za wafanyabiashara nchini. 

Taarifa hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati, Dkt. John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista
Mhagama, Waziri Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa
Viwanda na Uwekezaji Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, Angela
Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ahmad Chande, Makatibu Wakuu,
Makamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanakamati na
wataalam kutoka sekta mbalimbali za masuala ya kodi, biashara na uwekezaji.


Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema
Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na imeleta majibu ambayo yatatatua
changamoto za wafanyabiashara nchini na ameahidi kuwa Serikali imepokea
taarifa hiyo na itayafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na kamati
hiyo.

Kamati hiyo ambayo ilipewa siku 14, imefanya mapitio katika maeneo
mbalimbali ya kikodi, bandari, maeneo ya wafanyabiashara kwenye mikoa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...