Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WIZARA ya Mambo ya Ndani imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya TEHAMA vikiwemo Kompyuta, Mashine ya kudurufu na printa vyenye thamani ya Sh.milioni 44 kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula (WFP).

Akizungumza leo Juni 30, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo, Sudi Mwakibasi, amesema wanaishukuru WFP kwa utekelezaji wa maombi yao na vifaa hivyo ambavyo walikuwa wanavihitaji.

Ameongeza kwamba vifaa hivyo ufanisi kwenye idara yao huku akifafanua vifaa hivyo walivyopokea kutoka WFP vitatumika kwenye idara anayoisimamia.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri na Shirika hili, kwani mbali na kutoa chakula kwa wakimbizi waliopo kwenye kambi za hapa nchini bado wamekuwa wakifanya mambo mengine ya ziada na kuisaidia Serikali.

"Tunafahamu sasa hivi kumekuwa na changamoto ya fedha lakini bado WFP wameendelea kusaidia katika maeneo mbalimbali, tunawashukuru, " amesema.

Pamoja na mambo mengine katika kambi za wakimbizi kumekuwa na amani kwa sababu ya uhakika wa chakula kutoka WFP na sasa wameamua kusaidia katika elimu ya matumizi bora ya ardhi kwa wakimbizi."Kutokana na elimu hiyo, Wakimbizi saa wamekuwa wakizalisha chakula."

Pia Mwakibasi amesema kwa sasa ukienda kwenye makambi, kuna bustani za wakimbizi ambao wanazalisha mbogamboga na kusaidia upatikanaji wa chakula bora kwa ajili yao.

Awali Mkurugenzi na Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon amesisitiza wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wakimbizi wanakaa kwa amani na kupata mahitaji yao muhimu huku akifafanua wamekuwa na programu nyingi za kusaidia wakimbizi.

"Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania na kwamba vifaa ambavyo tumekabidhi vitasaidia katika utendaji kazi wa Wizara hiyo lakini wakati huo huo na kuwahudumia wakimbizi. "
Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon-Gibson(kulia) akimkabidhi Kompyuta mpakato( Laptop)Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo, Sudi Mwakibasi leo Juni 30, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon-Gibson(kulia) akimkabidhi Mashine ya kutolea nakala(Photocopy mashine) Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo, Sudi Mwakibasi leo Juni 30, 2023 jijini Dar es Salaam

Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon-Gibson (kulia) akizungumza leo Juni 30, 2023 katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani kabla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya TEHAMA kwa Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo, Sudi Mwakibasi(katikati).Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Fedha na Usimamizi wa miradi Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani.

Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon-Gibson(kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo, Sudi Mwakibasi leo Juni 30, 2023 jijini Dar es Salaam wakati WFP ikikabidhi vifaa vya TEHAMA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...