*Ni kwa Wanafunzi wa waliohitimu kidato cha Sita
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) kwa kinatarajia kutoa shahada ya kwanza ya Uuguzi kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kwa mwaka wa Masomo 2023/2024
Akizungumza katika maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mhadhiri wa Chuo hicho Dkt.Stewart Mbelwa amesema kozi ya shahada ya kwanza itaanza kwa Oktoba mwaka huu kwa uwezo wa wanafunzi 50.
Amesema kuwa AKU ilikuwa ikatoa shahada ya Uuguzi kwa wafanyakazi wa sekta ya afya walioko kazini ikiwa ilenga katika kujenga uwezo kwa watoa huduma wakiwa kazini na kuendelea kusoma.
Dkt.Mbelwa amesema kuwa kulingana kuwepo kwa mahitaji makubwa ya sekta ya afya kwa wauguzi ndipo waliamua kuanza na kozi ya shahada ya Uuguzi kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kwa viwango vya ufaulu vilivyoanishwa na TCU.
Aidha amesema kuwa Chuo kimejipanga katika kutoa elimu ya Uuguzi kwa viwango vinavyohitajika na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili wakihitimu kwenda kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Hata hivyo amesema kuwa AKU imejiimarisha kwa upande wa wahadhiri madaktari na Profesa katika kufundisha wanafunzi wataoanza kozi hiyo.
Amesema kuwa shahada hiyo ya Uuguzi itajikita katika ujuzi zaidi kuliko ya nadharia ambayo itamsaidia mwanafunzi kuwa sehemu ya kutatua changamoto pale atapohitimu na kwenda kutumikia kazi yake.
Dkt.Mbelwa amesema kuwa AKU katika uimarishaji wake wameweka maabara ya kiisasa ya kufundishia pamoja na vitendea kazi vingine ikiwa ni kuwasaidia wanafunzi watapohitimu kuwa ujuzi wa vifaa vya maabara.
Katika maonesho hayo Dkt.Mbelwa amewataka wazazi na wanafunzi kutembelea banda la Chuo Kikuu cha Aga Khan kupata elimu ya kozi wanazozitoa na kufanya uchaguzi.Watumishi tofauti za wahadhiri na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...