Chama cha Watoaji Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) kimefanya mkutano wa "Umuimu wa Vijana katika Sekta ya Nishati" unaolenga kuwapatia wanafunzi elimu pana kuhusu fursa zilizopo katika miradi ya nishati

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Nkurumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nishati, mgeni rasmi, Michael Mjinja, ambaye ni Kamishna wa Petroli na Gesi amesema, ni jambo la kuvutia kuona juhudi zinafanywa kuwaelimisha vijana wetu kuhusu miradi mipya na fursa zote zilizopo katika sekta ya Nishati.

"Mkutano wa "Umuimu wa Vijana katika Sekta ya Nishati" ni tukio linalolenga kuwapatia wanafunzi elimu pana kuhusu fursa zilizopo katika miradi ya nishati mipya kama vile mradi wa Gesi Asilia inayoyeyushwa (LNG), mradi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), pamoja na miradi mingine ya kisasa katika sekta ya hii" Amesema Minja

Amesema, kadri tunavyoendelea kuwa na wawekezaji wengi wanaokuja nchini mwetu basi ni vema pia kukawa na vijana wengi wenye uwezo wa kutambua fursa haraka na kuzitumia.

"Serikali inaleta miradi yote hii kwa lengo la kuboresha uchumi wetu na pia kutoa ajira kwa vijana, Kama vijana, mnapaswa kuwa tayari kushindana na watu kutoka vyuo tofauti katika sekta ya ajira..

Naye, Abdulsamad Abdulrahim mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya ATOGS, amesema wamevutiwa sana na jinsi wanafunzi vijana walivyo na hamu ya kupata elimu kuhusu miradi mipya. "Tupo hapa, tayari kutoa na kuwasaidia katika elimu yote mnayohitaji katika sekta ya nishati." Amesema

Katika hotuba yake, Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Martin Tiffen amesema; "Vijana ndio tumaini la nchi yoyote na tunafurahi sana kuwa sehemu ya jitihada hii kubwa, Timu yangu na mimi tunajivunia sana msaada wote na ari ya kujifunza zaidi kuhusu tunachofanya". Amesema Tiffen

Mradi wa EACOP una uwezekano wa kuwanufaisha wahandisi wa baadaye na labda hata wanafunzi kutoka idara zingine zote.

Mkutano huo wa "Umuimu wa Vijana katika Sekta ya Nishati" umehudhuriwa na wadau mbalimbali katika sekta ya nishati, ikiwa ni pamoja na Total Energies Marketing Tanzania, TPDC, TANESCO, na Wizara ya Nishat

Kamishna wa Mafuta na Gesi, Michael Mjinja akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaamu wakati wa kongamano umuhimu wa vijana katika sekta ya Nishati.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa bodi ya ATOGS, Abdulsamad Abdulrahim akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaamu wakati wa kongamano la Umuhimu wa vijana Katika sekta ya Nishati
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaamu wakisikiliza watoa mada wakati wa kongamano hilo
Waratibu na wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kongamano la Umuhimu wa vijana katika sekta ya Nishati
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...