Bendera zikiwakilisha mataifa ya Afrika ndani ya jengo la Ubalozi wa African Union Washington, DC, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani, Ijumaa July 7, 2023 na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza (hayuopo pichani ) aliongoza maadhimisho hayo. yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili wakiwemo Waheshimiwa Mbalozi waalikwa pamoja na mwenyeji wao Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Hilda Suka Mafudze.
Wa tatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Mabalozi waalikwa, wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Eswatini Mhe. Kennedy Fitzgerald Groening, wa pili ni Balozi wa Ukraine Mhe. Oksana Markarova na wa mwisho kulia ni balozi wa Kenya Mhe. Lazarus O. Amayo
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Elsie Kanza akiongoza maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023 katika jengo la Ubalozi la African Union Washington, DC.
kulia ni Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe, Hilda Suka Mafudze akitoa hotuba ya ufunguzi siku ya maadhimisho ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika jengo la Ubalozi la African Union Washington, DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akifuatilia hotuba hiyo.
Watatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023. Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijuamaa July 7, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...