Na BAKARI MADJESHI, Michuzi TV

Winga raia wa Msumbiji, Luís José Miquissone rasmi amerejea kwenye Kikosi cha Simba SC, amesajiliwa Kikosi hapo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Abha FC ya Saudi Arabia alipokuwa kwa mkopo wakati akiwa na Al Ahly SC ya Misri.


Simba SC imetangaza kumrejesha Miquissone Kikosini ikiwa na lengo la kuboresha Kikosi hicho ambacho kilikosa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo.


Luís Miquissone amerejea Simba SC msimu huu wa 2023-2024, aliondoka na kusajiliwa na Al Ahly SC mwaka 2021 ambapo baada ya usajili huo Al Ahly walimtoa kwa mkopo katika Klabu ya Abha ya Saudi Arabia.


Miquissone amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na uwezekano wa kuongeza mkataba mwengine Kikosini hapo Msimbazi.


Hadi sasa Simba SC imesajili wachezaji Willy Essomba Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda, Aubin Kramo Koume kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone kutoka Klabu ya Coton Sports ya Cameroon, Fabrice Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan.


Wachezaji wa ndani walisajliwa hadi sasa ni Hussein Kazi, Abdallah Hamis na Shaaban Iddi Chilunda.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...