KATIBU  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amewasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mapema leo asubuhi, tayari kuelekea jijini Arusha kufanya mkutano  mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi ya Julai 22,2023.

Akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wassira na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Chongolo baada ya kuwasili uwanja wa ndege, amelakiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Katika mkutano huo wa leo, pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Chongolo ataelezea hatua kwa hatua  usahihi wa makubaliano ya uwekezaji kwa ajili ya kuboresha uendeshaji na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti, ili kuongeza, tofauti na ilivyo sasa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...