*Yabainisha moja ya ajira ni wahitimu kuanzisha kampuni ya ushauri wa masuala ya kodi.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Chuo cha Kodi kimesema kuwa wanafunzi wanaosoma chuo hicho uwanja wa mkubwa wa kuajiri au kuajiri kutokana kuwepo kwa uhitaji rasimali watu wenye ujunzi wa kodi.
Hayo ameyasema Mkuu wa Uhusiano wa Chuo hicho Oliver Njunwa wakati akizungumza kwenye maonesho 18 ya vyuo vikuu yanayondelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa wanafunzi wakihitimu katika Chuo hicho anaweza kuanzisha kampuni ya ushauri wa kodi katika kampuni zilizopo nchini na nje ya nchi.
Njunwa amesema kuwa Chuo hicho kinafundisha kwa uweledi kutokana na wanafunzi hao wanatarajiwa kutumikia taifa kwa katika masuala ya kodi.
Aidha amesema kuwa soko la ajira kwa sasa lipo wazi kwa wataalam wa kodi kutokana na fursa nyingi ambayo inatokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta binafsi vikiwemo viwanda.
"Tunaamini wahitimu wanaotoka katika chuo chetu wanakuwa wameiva pasipotiliwa shaka kutokana na uweledi uliojengwa katika chuo hicho"amesema Njunwa Mkuu wa Uhusiano Chuo cha Kodi.
"Tangu maonesho haya yaanze tumekuwa tukipokea maswali mengi kutoka kwa wanafunzi na kwa wale wanaotarajiwa kujiunga na Chuo cha Kodi, ambapo swali lao kubwa wanauliza fursa za ajira watakapohitimu,"
"Wengi wanafikiri ukishahitimu hapa ni lazima ufanye kazi TRA, ndiyo maana tuna kozi zinatolewa kwa vijana waliyomaliza shule za sekondari, mafunzo tunayoyatoa yanamuwezesha anapohitimu aweze kufanya kazi kwa weledi kutokana na misingi anayoelekezwa," amesema Njunwa
Pia, amasema muhitimu katika chuo hicho kutokana na taaluma waliyoipata ni sawa anaweza kuajiliwa TRA ambapo hiyo ni sehemu moja, lakini anaweza kuajiliwa kwenye taasisi zingine za serikali, kwa ajili ya kuwashauri kuhusu masuala ya sera za kodi.
"Mwanafunzi akishahitimu tayari anakuwa ni mtaalamu wa kodi kwa hiyo anaweza kuajiliwa kwenye taasisi za serikali, kwenye mashirika au kampuni binafsi ambayo yanafanya biashara, kumbuka wajibu mkubwa wa TRA ni kukusanya mapato sahihi ya serikali,"
"Hivyo, hawa wataalam wameandaliwa kwa ajili ya kuisaidia TRA ili iweze kukusanya mapato na kuweza kuongeza mapato ya serikali. Hapa Tanzania tunawawekezaji wengi, ambapo wakishafika nchini lazima watalipa kodi, watalipaje kodi sahihi, ni kwa kupata wataalam walio sahihi, kwa hiyo fursa za ajira zipo nyingi,"amesema
Pia, amesema fursa nyingine ipo kwa wafanyabiashara ambao wanajikadilia kodi ambapo wao wanahitaji wataalam, kwa hiyo vijana waliyomaliza katika chuo hicho wanaweza kuwajiliwa na wafanyabiashara hao na kuweza kuwakadilia kodi kwa usahihi.
Mkuu wa Uhusiano wa Chuo cha Kodi Oliver Njunwa akizungumza na waandishi habari kwenye Banda la Chuo katika Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...