Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limesema Katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya walinzi wa viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza mtu yeyote ambaye si askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za majeshi  ambapo ameongeza kuwa sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza Pia alisema Misime.

Pia amesema Jeshi la Polisi Tanzania linawataka wale wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Misime ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...