Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya FOODEX imetangaza mkakati mpya wa kuboresha utoaji wa huduma za chakula na hoteli nchini Tanzania lengo kuu likiwa ni kuchangia kujiada za serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa FOODEX Safa Erzurumlugil, amesema kampuni yake imeona kwa vile Tanzania imeboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji, ni muda mwafaka kushiriki katika juhudi hizo za kuiunga mkono serikali ya Tanzania.
Amesema njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kuboresha huduma katika maeneo ambayo kampuni yake ina uzoefu nayo.
“Tumedhamiria kufanya mapinduzi katika utoaji wa huduma za chakula na hoteli nchini Tanzania na kuzifanya zikidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa na pia kwa lengo la kuvutia wageni, watalii na wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.
" Lengo ni kutoa huduma bora za vyakula zinazowavutia wageni wengi, wanaokuja kufanya biashara na kutalii hapa kwetu,” amesema Safa Erzurumlugil.
Ameongeza kwamba FOODEX imeona ni vizuri kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akiinadi kwa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini na kuboresha huduma za jamii.
“Tumejizatiti kuisaidia Serikali kutimiza ndoto zake kwa kufanya mapinduzi na maboresho makubwa katika huduma za chakula na hoteli…kutoa huduma zenye viwango na bora kwa wageni, watalii na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.”
Katika mazingira ambayo serikali imeweka mikakati dhabiti na ya muda mrefu kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza, utoaji wa huduma nzuri ya vyakula zinazokubalika kitaifa na kimataifa ni jambo lisiloepukika.
“Ukuaji wa biashara na uwekezaji utahitaji utoaji wa huduma bora za chakula na huduma zingine zinazoendana mahitaji ya soko. Ndiyo maana Foodex imekuja na mkakati mpya ambao utahakikisha Watanzania na wageni wanaofanya biashara nchini wapata huduma bora na tuko hapa kwa kazi hiyo.”
Akielezea zaidi kuhusu huduma zao, mkuu huyo wa kampuni ya Foodex amesema kampuni yake itatoa huduma ambazo zitatumiwa na aina zote za matukio ya kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa na kwamba wateja (watu binafsi, taasisi za serikali, mashirika ya kitaifa na kimataifa etc) watapata uzoefu wa aina yake (wa vyakula) kwa sababu FOODEX wamejipanga kutoa huduma tofauti na zenye ubora.
“Tuna timu ya wapishi wazoefu, waandaji wa mipango na wafanyakazi wanaotoa huduma zao kwa kushirikiana na kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kweli huduma tunazozitoa zinatufanya tuonekane kampuni ya kipekee katika utoaji wa huduma bora za chakula kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu.
"Katika huduma za chakula tunazozitoa tunatumia viambato vyenye ubora na hivyo wateja wetu wana uhakika wa kupata chakula chenye hadhi na ambacho wanaweza kumudu gharama zake,” amesema.
Alieleza kwamba aina ya huduma ambazo walikuwa nazo ni pamoja na huduma zinazoendana na upishi wa kimataifa kama vile Italia, India, China, na milo mbambali inayolenga mahitaji ya wateja wao.”
Kwa mujibu wa Safa Erzurumlugil, FOODEX imejipanga kutoa huduma zenye ubora na katika mapishi ya aina mbalimbali za vyakula vinavyoweza kutolewa kwa matukio ya kitaifa, kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa, warsha, semina, mafunzo, matamasha na sherehe mbalimbali.
“FOODEX imekuja na mikakati itakayoiwezesha kushindana kikamilifu kwa kutoa huduma nzuri za chakula na hoteli Tanzania, huki ikizingatia sera, sheria, kanuni, usalama wa afya na kuweka mazingira katika hali ya usafi.”
Home
Unlabelled
KAMPUNI YA FOODEX YATANGAZA MKAKATI MPYA WA KUBORESHA UTOAJI CHAKULA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...