Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF – Inkotanyi) Ndugu
Wellars Gasamagera (kushoto) leo tarehe 1, Julai 2023 katika Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mara baada
ya mazungumzo hayo Katibu Mkuu huyo wa Chama cha RPF Inkotanyi pamoja na
ujumbe wake watatembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR pamoja
na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha kwa mfipa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongoza mazungumza baina yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF – Inkotanyi) Ndugu Wellars Gasamagera (kulia) pamoja na ujumbe wake leo tarehe 1, Julai 2023 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Ofisa Mshauri Ofisi ya Rais Rwanda Ndugu Ndahiro Alfred (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF – Inkotanyi) Ndugu Wellars Gasamagera leo tarehe 1, Julai 2023 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Kada wa RPF-Inkotanyi Ndugu Tom Ndahiro mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF – Inkotanyi) Ndugu Wellars Gasamagera leo tarehe 1, Julai 2023 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...