NA PAUL WILLIUM, MOSHI.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Casper Casper amesema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kufanya kazi lakini wamekuwa hawafanyi hivyo na badala yake wamekuwa wakichunguza mapungufu yaliyopo nchini na kuanza kuyasemea vibaya ili kuichafua.
Katibu mkuu huyo alitoa kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kutathimini utendaji kazi wa Jeshi la Uhamiaji kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 kilichofanyika katuja chuo cha Uhamiaji kikanda (TRITA), mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa, kama nchi ni lazima kujipanga kimkakati na kuweza kujua wapinzani wa kiuchumi wanafikiri nini juu yetu na kuwa na maono ya kiintelijensia na kujipanga kwa miaka ya mbele ili kukuza uchumi wa nchi.
“Kunawatu wamejipanga kimkakati wanaweza kuja na kutafuta kazi ndani ya nchi yetu baada ya kuja kufanya kazi ile waliyoomba wanaanza kuchunguza nchi hii inamapungufu gani na kuanza kuyasemea vibaya na kuanza kuichafua nchi yetu sisi kama vyombo vya usalama ni lazima tujue hao ni wakinanani” alisema Casper.
Alisema kuwa, wao watu wanazungumza vibaya kuhusu jeshi la Uhamiaji na kuwataka kujirekebisha kama mambo hayo yanayosemwa yapo lakini kama yanasemwa kwa nia ya kulichafua Jeshi hilo na kulionea huyo mtu sio rafiki.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa, nchi ikiwa salama na wananchi wakiwa salama wanakuwa na uhakikana maisha na mali zao hivyo watafanya shughuli za maendeleo na kuwataka kudumisha ili kuwa na mahusiano mazuri na wageni wanaoingia nchini.
Casper aliwataka Makamanda wa Uhamiaji mikoa kutosita kuwachukulia hatua pale askari aliyechini yake anapofanya makosa na kuwataka kujiamini kwani wao ndio viongozi wa kuwaongoza na kuwasimamia askari wa chini.
“Kiongozi unapaswa kuwa na uwezo wa kuonya au kuchukua karipio pale unapoona kunakosa usijisahau na wewe ukaanza kufanya mambo ambayo sio sawa soma mwongozo ni makosa gani ambayo unaweza kusimamia na kuchukua hatua” alisema Casper.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala alisema kuwa, katika kuhakikisha Jeshi la Uhamiaji linatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa wamekuwa na utaratibu wa kufanya vikao vya kujitathimini utengdaji kazi wetu kila mwaka.
Dkt. Anna alisema kuwa, pia kikao hicho kinatumika kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo ya Jeshi la Uhamiaji na kupitia vikao hivyo wameweza kuimarisha umoja, uwaajibikaji pamoja na kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Jeshi la Uhamiaji.
Alisema kuwa, ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Uhamiaji katika kikao hicho wamewajumuisha makamishina wa uhamiaji, makamanda wa uhamiaji wa mikoa yote nchini na wakuu wa divisheni.
“Katika kikao kazi hiki tutapata fursa ya kusikiliza mada na taarifa mbalimbali za utendaji kazi ya kuanzia kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 kutoka kwa makamanda wa uhamiaji mikoa yote na kujitathimini kwa kina juu ya utendaji kazi yetu” alisema Dkt. Anna.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...