Na. Damian Kunambi, Njombe.
Wananchi
wa kata ya Madilu iliyopo Wilayani Ludewa Mkoani Njombe wamelalamikia
vipimo vya viazi wanavyohitaji wanunuzi ambapo wamekuwa wakihitaji ujazo
wa Lumbesa kitu ambacho kinawapa hasara wakulima hao.
Wakitoa
malalamiko hayo mbele ya Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga mara
baada ya kufika katani hapo na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali
vya kata hiyo ikiwa ni ziara ya kupita kijiji kwa kijiji katika jimbo
hilo iliyolenga kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi.
Fabian
Msigwa ni miongoni mwa wananchi hao amesema japo kilimo cha mwaka huu
wamekifanya kwa urahisi kutokana na kupata mbolea za ruzuku kutoka
serikalini lakini wanapokuja kuuza mazao hayo wanakumbana na changamoto
hiyo inayopelekea waone uraisi walio upata wa mbolea ya ruzuku ni sawa
na bure.
"Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kutupa ruzuku ya mbolea ambayo imetufanya tulime kwa urahisi sana,
ila Mbunge wetu tunaomba ufikishe salamu hizi za lumbesa zinatuumiza
wakulima na kutufanya tuone kama ruzuku ya mbolea inajifidia kwenye
vipimo vya lumbesa ya viazi". Amesema Msigwa.
Aidha kwa upande
wake Mbunge Joseph Kamonga amesema agenda hiyo ya lumbesa wataipeleka
bungeni kwa kushirikiana na wabunge wenzie wa majimbo ya mkoa wa Njombe
lakini pia wataungana na wabunge wa mkoa wa Mbeya ambapo watamuomba
waziri wa kilimo Hussein Bashe kuweka mfumo usio umiza wakulima
ikiwezekana viazi hivyo kupimwa kwa kilo.
" Wakati wa bunge la
akina Makweta na Mathias wale walikuwa na utarabu wa kuungana na
kusukuma agenda kwa pamoja hivyo hii hoja ya lumbesa mtanisikia bungeni
nikiisemea kwani haiwezekani wakulima mshindwe kunufaika na mazao yenu
waje wanufaike watu wengine" Amesema Kamonga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...