NA VERO IGNATUS,ARUSHA
Wizara ya Utamadulni Sanaa na michezo kupitia Baraza la kiswahili la Taifa(BAKITA) pamoja na kampuni ya Africa sport Agency imeandaa marathon msimu wa kwanza ikiwa ni programu za kutangaza lugha ya Kiswahili kutumia matamasha michezo ili kukuza lugha hiyo nakuongeza chachu ya matumizi kwa wageni wafikapo nchini.
Mbio hizo za masafa za Swahili ambazo zimefanyika jijini Arusha nakushirikisha wageni kutoka mataifa mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya kiswahili duniani ambapo kilele chake kitakuwa julai 7. 2023 Zanzibar.
Akizungumza baada ya kuongoza mbio hizo Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma alisema kuwa mbali na kukuza lugha adhimu ya kiswahili pia michezo inajenga Afya na kuepusha magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuepukika
Siku hii ya kuanzishwa rasmi juma la kiswahili hapa nchini limetokana tangazo la Shirika la elimu Sayansi na Utamaduni Duniani UNESCO katika mkutano wake wa 41 kuitambua lugha ya kiswahili kama kimataifa, aidha ametoa pongezi kwa baraza la kiswahili Bakita ,kwa lengo kuleta ari na mwamko katika lugha, sambamba na kumuunga mkono Mhe. Rais kwasababu amewekea nguvu nyingi na kuhakikisha kuwa Arusha inapata sifa inayostahili kukuza sekta ya Utalii
Mbio hizo zimewaleta watu pamoja, hivyo Mwinjuma amesema kutoka Wizarani wao wataendelea kukifanya kiswahili kuwa bidhaa katika utalii, ''Itafika mahali watalii wanapokuja nchini watakuwa wanafuata lugha ya kiswahili kama vile ambavyo wanafuata wanyama, na miongoni.mwa vifurushi tutakavyoviuza kwa watalii ni kiswahili ili kiweze kukua''.Alisisitiza
Katibu Mtendaji wa Baraza la kiswahili Bakita, Consolata Mushi amesema Baraza la kiswahili Bakita limendaa mbio za masafa za Swahili kwa mara ya kwanza mkoani Arusha ikiwa ni kuhanikiza Juma la Kiswahili ambalo linatarajiwa kilele kufanyika tarahe 7 julai Zanzibar.
Bi Consolata amesema kuwa Kiswahili ni lugha ya umoja na mawasiliano kwa watu wengi sana Barani Afrika na nje ya Afrika,lakini tunataka kuonesha kwa jinsi gani Kiswahili kilivyo na uwezekano mkubwa katika zama za kidijitali.
Awali Naibu waziri Hamis Mwinjuma alitoa zawadi kwa washindi wa mbio za masafa za Swahili huku akiwataka viongozi nchini kutumia muda wao kukibidhaisha kote Afrika mashariki na duniani.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akizungumza katika katika uzinduzi wa mbio kwaajili ya kuelekea kilele cha kiswahili julai 7,2023,amesema kuwa jitihada zote hizo za kukuza Kiswahili zinakwenda sambamba na kuunga mkono juhudi za mhe.Rais kutokana na filamu ya royal tour,ambapi Arusha imekuwa wanufaika wakubwa ambapo wanaweza kutangaza lugha ya kiswahili duniani kupitia Utalii.
Ikumbukwe Siku ya lugha ya kiswahili duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 7 Julai tangu ilipopitishwa rasmi na UNESCO miaka mwili iliyopita 2022, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, yaliyoandaliwa kwa pamoja na ujumbe wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa AFrika, SADC, Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na wadau wengine kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili.
Kuzungumza Kiswahili ni kurahisisha mawasiliano na kuunganisha watu wa mbalimbali kwani Kiswahili ni kielelezo cha kipekee cha desturi na utamaduni wa kiafrika na ustaarabu pamoja na fikra za watu,Kiswahili kina nafasi kubwa katika mawasiliano, sayansi na teknolojia kwa sababu kinawezesha kupata habari, elimu, mawazo mapya pamoja na kumiliki sayansi na teknolojia. Kwa njia. Baraza Kuu la UNESCO lilipitisha mwezi Novemba mwaka 2021 bila kupingwa azimio la kutangaza tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.
Maudhui ya mwaka huu ambayo ni: “Kuibua uwezo wa Kiswahili katika zama za kidijitali kwa sababu tunauhakika kwamba Kiswahili kinaweza kutumika kama daraja kuunganisha jamii mbalimbali na kuwezesha ujumuishwaji katika ulimwengu wa kidijitali.”
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akimkabidhi Naibu Waziri T-shirt katika uzinduzi wa mbio zilizofanyioa Meru kwaajili y a kuelekea kilelel cha kiswahili tar 7/7 sambamba nanhayo kutokana na filamu ya royal tour
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma akizungumza katika uzinduzi wa mbio za masafa zilizofanyika Meru kwaajili ya kuelekea kilelel cha kiswahili Zanzibar Julai 7,2023
“Kiswahili ni lugha ya umoja na mawasiliano kwa watu wengi sana barani Afrika na nje ya Afrika,Lugha hii Adhimu ni ya kwa sita bora duniani,pia hutumika kama daraja kuunganisha jamii mbalimbali na kuwezesha ujumuishwaji katika ulimwengu wa kidijitali,Kiswahili kina uwezo mkubwa katika zama za kidijitali, hivi sasa jamii zetu zimeunganishwa ni muhimu kila mtu kuwa na fursa ya nyenzo hizo na tunazihitaji kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na mijadala katika jamii zetu na kila mtu kushiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...