MAHAKAMA inategemea kutumia Sh. bilioni 207.3, kujenga vituo vipya jumuishi tisa na mahakama za mwanzo 60, ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza miundombinu na kusogeza huduma kwa wananchi.

Aidha, mhimili huo upo katika hatua za mwisho kuanza kutumia akili bandia (artificial intelligence), katika kuandika hukumu.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Profesa. Elisante Ole Gabriel, ameyasema hayo wakati akizungunza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema, kituo kimoja jumuishi kitajengwa visiwani Pemba.

“Kwenye miundombinu tuna mahakama 960 za Mwanzo, mahakama 134 za Wilaya, Mahakama 30 za Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu 19, Mahakama 1 ya Rufani yenye subsidiary 16,” alisema.

Kuhusu matumizi ya akili bandia, Prod. Ole Gabriel amesema maboresho ya mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), yapo katika hatua za mwisho kukamilisha kazi hiyo.

“Kwenye TEHAMA tunakwenda vizuri na tunategemea hivi karibuni kufanya majaribio ya kuandika hukumu kwa akili bandia katika mahakama kuu divisheni ya biashara,” amesema.

Katika hatua nyingine, Prof. Ole Gabriel amesema kituo cha huduma kwa wateja cha mahakama kimefanikiwa kusikiliza na kushughulikia changamoto 2,429 za wananchi kati ya 2,444 zilizopokelewa.

Ameongeza kuwa mfumo wa TEHAMA wa kusajili kesi umepunguza muda wa kuwasilisha mashauri na kuondoa kero kwa wananchi.

Mtendaji huyo ameishukuru serikali kwa kujenga jengo kubwa la makao makuu ya Mahakama jijini Dodoma ambalo limegharimu Sh. bilioni 129.7 ambalo ni la sita kwa ukubwa duniani.
Prof. Ole Gabriel akizungumza Wakati alipotembelea banda la Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi katika maonyesho ya Sabasaba 2023.

Prof. Ole Gabriel akipata maelezo kutoka Banda la Kurugenzi ya Usimamizi, Ukaguzi wa Huduma za Mahakama, Maadili na Malalamiko. Kulia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi anayehudumu katika Kurugenzi hiyo, Lome Mwapemela.

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Mipango- Mahakama ya Tanzania, Gladys Qambaita aliyekuwa akimueleza kuhusu mipango na maboresho mbalimbali ya Mhimili huo.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania. Mahakama ya Tanzania inashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...