Na. Damian Kunambi, Njombe
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ameahidi kuchangia mabati 230 katika shule ya sekondari Lubonde ili ziweze kusaidia katika ujenzi wa mabweni ya shule hiyo.
Akitoa ahadi hiyo mbele ya mkutano wa hadhara katika vijiji vya Masimbwe, Mkiu Pamoja na Kiyombo mara baada ya wananchi hao kueleza changamoto ya uwepo wa mabweni hayo ambapo wananchi hao wameanza kuchangia ujenzi wa bweni moja.
Kamonga amesema sanjali na kuchangia bati hizo lakini tayari amefanya jitihada za kuiomba serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii ( TASAF) ambao nao wameahidi kuunga juhudi hizo kwa kujenga bweni moja.
Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Edga Mtitu alimshukuru mbunge huyo kwa jitihada mbalimbali za maendeleo anazofanya ambapo hivi karibuni serikali imewaingizia fedha kiasi cha sh. Mil. 100 kwaajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
Ikumbukwe kuwa shule hiyo ni mpya ambayo imeanza kupokea wanafunzi mwezi January mwaka huu na kuondoa adha kwa wanafunzi wa kata hiyo waliokuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata elimu hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...