Na Muhidin Amri, Tunduru


MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka,ametoa msaada wa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni 2.5 kwa familia yenye mapacha watatu inayoishi kijiji cha Mkapunda wilayani Tunduru ili iwaingizie kipato kitakachosaidia kwenye malezi ya watoto wao.

Baba wa watoto hao Hamis Shaibu alisema,baada ya kujaliwa kupata watoto mapacha wanne alilazimika kumuomba Mbunge pikipiki ili iwasaidie kulea watoto kwa kubeba abiria kutokana na changamoto ya maisha waliyonayo.

Alisema  hana kazi wala shughuli yoyote ya kumuingizia kipato,jambo ambalo lingeweza kumsumbua katika malezi ya watoto wake hasa ikizingatiwa kwamba yeye ndiyo kichwa cha familia licha ya mama wa watoto hao Judith Sichawe ni Mwalimu wa shule ya msingi.


Amemshukuru Mbunge kutokana na msaada huo,na kuhaidi kutumia pikipiki hiyo kufanyia biashara itakayowaingizia kipato ambacho kitakwenda kupunguza ukali na ugumu wa maisha kwenye safari ya malezi kwa watoto wao.

Aidha,amewaomba wasamaria wengine kuendelea kuwasaidia katika malezi na matunzo ya vijana wao kwa kutoa walichanacho kwa sababu watoto hao bado wana uhitaji wa vitu vingi.

Naye mama wa watoto Judith Sichawe alisema,alifanikiwa kujifungua mapacha wanne hata hivyo kwa bahati mbaya mtoto mmoja amefariki Dunia tangu mwezi Septemba mwaka jana na sasa wamebaki watatu wenye umri wa mwaka mmoja na miezi 2.


Mbunge wa viti maalum Mariam Nyoka alisema,amelazimika kutoa msaada huo  kwa kuwa anatambua ugumu wa kulea na kutunza watoto mapacha kwa wakati mmoja na changamoto ya kimaisha inayoikabili familia hiyo.


Alisema,hiyo ni mara ya pili  kuitembelea na kutoa msaada kwa familia hiyo yenye jukumu kubwa la kulea watoto wao  hadi pale watakapokuwa watu wazima na kuanza kujitegemea.


Kwa mujibu wa Nyoka,kulea watoto mapacha watatu  ni kazi ngumu inayohitaji kipato kikubwa,na yeye kama sehemu ya jamii ameona ni vyema kuisaidia familia hiyo pikipiki ambayo itakuwa  chanzo kikubwa cha kuwaingizia kipato.

Mkazi wa kijiji cha Mkapunda wilayani Tunduru Hamis Rashid kushoto,akipokea kofia ngumu ya kuendeshea Pikipiki kutoka kwa Mbunge wa viti maalum mkoani Ruvuma Mariam nyoka aliyewapatia pikipiki familia ya Rashid yenye watoto mapacha watatu ili iweze kuwaingizia kipato kwa ajili ya kulea na kuwatunza watoto wao. Hamis Rashid kulia na mkewe Mwalimu Judith Sichawe katikati na watoto wao mapacha watatu wakiwa na furaha baada ya kupokea msaada wa Pikipiki kutoka kwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka(hayupo pichani)ili iwasaidie kuwaingizia kipato na matunzo ya watoto wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...