Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini (Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti) Daniel Sillo ametimiza ahadi yake ya kukabidhi mashine za kuchapisha katika shule za Sekondari Maganjwa na Arisaayo ili kusaidia katika kuchapa mitihani.Akizungumza wakati akikabidhi mashine mbili katika shule hizo, amesema kuwa hadi sasa ameshatoa mashine zaidi ya 16 kwenye shule za Sekondari na kwamba hadi mwaka 2025 atakuwa amekamilisha kugawa na kwenye shule za Msingi.
Sillo amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazo wakabili kwa kadri atakavyoweza.
Katika hatua nyingine, amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayofanya ya kufundisha na kuongeza ufaulu katika wilaya ya Babati.
Nao Madiwani wa Kata ya Arri na Dabil wamemshukuru Mbunge huku wakisema kuwa kitendo cha kutoa msaada huo kinaonesha ni jinsi gani anaunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassani ya kujenga miundo mbinu bora ya elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma bila shida
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...