NA BALTAZAR MASHAKA, ILEMELA

MBUNGE wa Ilemela (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk.Angeline Mabula ameanika mafanikio lukuki ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye sekta za afya,elimu,maji na miundombinu ya barabara yaliyotokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Akiwasilisha utekelezaji wa ilani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,leo Dkt.Mabula amesema katika kipindi cha Novemba 2020 hadi Disemba 2022,miradi ya maendeleo katika Jimbo la Ilemela imegusa maeneo mbalimbali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,katika kipindi cha miaka mwili hadi Machi 2023 ilipokea shilingi 46,089,606,519.60 zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika huduma za jamii kwenye sekta za elimu, maji,afya,barabara na kiuchumi katika Jimbo la Ilemela.

Dkt.Mabula amefafanua kuwa sh.bilioni 13.8 zilitumika kujenga Stendi ya Mabasi, Nyamhongolo,bilioni 1.940 za Uviko-19 zikiwemo za pochi la mama,zilijenga madarasa 207 ya shule za sekondari 26,bilioni 4.006 za miradi ya kupunguza umasikini ziliwezesha wananchi wenye kipato cha chini kukabiliana na umasikini.

“Hakika tunajivunia kuwa na Rais mwenye maono na mwenye kujali ustawi wa watu anaowaongozana,ametoa fedha nyingi kuhakikisha huduma za jamii zinawafikia Watanzania wote kwa wakati,”amesema.

Mbunge huyo wa Ilemela amesema elimu bila malipo kiasi cha bilioni 4.403 kilitumika kwa shule za sekondari huku elimu ya msingi ikipatiwa sh. bilioni 2.136 ambapo sekta ya afya ilipata sh.bilioni 1.350 za tozo na kutoka serikali kuu ili kujenga hospitali ya wilaya na zahanati za Masemele,Lumala,Nyamadoke na kituo cha Afya Buzuruga.

Aidha kipidi kifupi cha miaka miwili chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia sekta ya elimu imeboreshwa kwa kujenga shule mpya tano za msingi na miundombinu mingine katika kata sita kwa sh. milioni 226.5 za mapato ya ndani.

“Ilani inaitaka serikali kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu,kuhifadhi na kuendelezaa mazingira ya shule ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa kutoka 600 hadi 1000 ifikapo 2025,ili kupunguza uhaba wa madarasa na kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kwenda shule na kurudi,shule za sekondari sita za kata za Bugogwa,Buzuruga,Kahama,Shibula,Semba na Nyamhongolo zimejengwa,”amesema Dk.Mabula.

Waziri huyo wa Ardhi amesema ili kurahisisha uboreshaji wa miundombinu mipya ya shule za sekondari na msingi,ofisi ya mbunge imeendelea kuchangia vifaa vya ujenzi kuunga mkono juhudi za wananchi.

Pia serikali katika kuhakikisha inatoa huduma bora na salama za maji safi imesogeza huduma hizo karibu na wananchi, kuhakikisha kampeni ya kumtua Mama Ndoo Kichwani inatekelezwa imejenga miundombinu mikubwa kwenye makazi likiwemo tenki kubwa la maji Kiseke, lililogharimu sh.bilioni 365.580.

"Mradi wa tenki la maji Buswelu lenye uwezo wa kuhifdhi lita milioni tatu za maji umetekelezwa kwa bilioni 5.106 ili kuboresha huduma hiyo eneo la Buswelu na tayari unawahudumia wananchi.Yote haya sijayafanya binafsi bali Rais katika kuleta maendeleo na kuwapunguzia kero wananchi katika huduma za jamii,”ameeleza.Dkt.Mabula.


Amesema sekta muhimu ya barabara katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii,mbunge huyo ameendelea kuiunga mkono serikali na Chama Cha Mapinduzi ili kujibu kiu ya wananchi akifungua barabara za mtaa kwa mtaa ambapo km 26.7 zimefunguliwa katika mitaa 21 kwa zadi ya sh.milioni 18 kwa usimamizi wa TARURA.

Kwa mujibu wa ibara ya 122 (h) na 18 (b)(iii) zinazoielekeza serikali kubuni na kuibua miradi ya kimkakati ya kuboresha huduma za wananchi katika mamlaka za mitaa ili kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi wa ruzuku,mbunge alihakikisha miradi yote iliyobuniwa inatekelezwa ukiwemo wa Stendi ya Nyamhongolo uliogharimu sh.bilioni 26.65.

Mgeni rasmi katika wasilisho hilo la utekelezaji wa Ilani,Katibu wa Itikadi na Uenezi,Sophia Mjema amesema chini ya Rais Dk. Samia,mafanikio ya haraka kwa muda mfupi wa uongozi wake mahiri na kutaka kuona maendeleo ya wananchi wake yamepatikana tangu uchaguzi mkuu wa 2020.
“Mbunge ameeleza yote yaliyoelekezwa kwenye ilani na kuyasimamia kwa vitendo,sote ni mashahidi kazi kubwa imefanyika Ilemela kwa asilimia.Hivyo basi viongozi wa CCM wanajukumu kubwa la kuelekea chini kwa wananchi kujibu kero zao hasa wana chama,tusipofanya hivyo tutaonekana watu wa porojo na kwa tuliyotekeleza Mwenyekiti wetu wa Chama anaahidi na kutekeleza pale pale,”amesema Mjema. sssss


Katibu wa NEC (CCM),Itikadi na Uenezi,Sophia Mjema, wa pili kutoka kushoto, akiwasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, leo tayari kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020-2025 katika Jimbo la Ilemela,kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM), Dkt. Angeline Mabula.Mbunge wa Ilemela (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miaka miwili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...