Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalist Lazaro amesema migogoro mingi inayotokea kati ya kijiji na kijiji au kata kwa kata inatokana na maslahi binafsi ya viongozi wa maeneo husika baada ya kuibuka kwa fursa mbalimbali za kiuchumi.

Hayo ameyasema baada ya kuwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 / 2025 kwa wilaya ya lushoto..

Mkuu huyo wa wilaya amesema kulingana na migogoro hiyo ya wilaya mbili watahakikisha wanaitatua kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya korogwe Joketi Mwegelo.

"Migogoro mingi ya Kijiji kwakijiji kata Kwa kata inatokana na maslahi binafsi ya viongozi hasa inapotokea fursa kama eneo likigundulika kuwa na madini au eneo la msitu au muwekezaji akitaka eneo Hilo"Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wao Madiwani wa kata mbalimbali zilizopo Lushoto ambao ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo walisema kuwa migogoro hiyo ya mipanga inawakosesha mapato katika kata zao.

Hozza Mandia Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba alikiri kuwepo na migogoro mingi ya mipaka katika vijiji vyao na kata zao lakini akabainisha migogoro hiyo inasanabishwa na eneo linalolimwa zao la mkonge na eneo linapogundulika na madini .

Mandia alieleza kuwa migogoro hiyo imekuwa ikiwasabishia kukosekana kwa mapato ya uhakika kutokana panapotokea mgogoro wa mipaka wanaofaidika ni wa kijiji kimoja kati ya hivyo vyenye migogoro.

Nae Diwani wa Vuga Jumaa Dhahabu yeye alienda mbali zaidi kutaka serikali iingilie kati migogoro hiyo ambayo alisema nichangamoto ya muda mrefu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...