Na Mwandishi Wetu, Butiama

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amemtaka Meneja anayesimamia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “B” Wilaya ya Butiama lililotengewa kiasi cha Shilingi milioni mia nane kutoka Serikalini kuhakikisaha kuwa anaharakisha ujenzi wa jengo hilo ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na ubora.

Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo wakati alipotembelea ujenzi wa kituo hicho na kukagua shughuli  zinazoendelea katika mradi huo.

Akiwasilisha taarifa ya mradi Meneja wa mradi Inspekta Charles Thobias amesema kuwa mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja “B”  Wilaya ya Butiama unatekelezwa na  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ulianza rasmi tarehe 6 Mei, 2023 na unatarajiwa kukamilika mwezi  Septemba 2023.

“Mradi huu unatekelezwa kwa njia ya nguvu kazi “Force Account” fedha zilizopokelewa hadi tarehe ya leo ni Shilingi milioni mia tano ambapo kati ya hizo fedha zilizotumika hadi tarehe 30 Juni, 2023 ni Shilingi milioni mia mbili arobaini na nane.”Alisema Inspekta Charles

Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya baadhi ya miradi inayotekelezwa hususani katika Mkoa wa Mara kutokamilika kwa wakati kutokana na kukosekana kwa usimamizi na ufuatiliaji  wa mara kwa mara kutoka kwa wasimamizi wa miradi hiyo.

“Mheshimiwa Rais alishatulaumu watu wa Mara kwamba miradi ya Mkoa wa Mara huwa haimaliziki. Hii ni miradi iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na wasimamizi ni ninyi wenyewe na sio wasimamizi kutoka nje. Ninyi ni Askari pelekeni jengo hili Kiaskari. Isifike mwezi wa tisa na fedha zimetolewa na Serikali ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan halafu hammalizi kwa wakati.” Alisema Naibu Waziri Sagini.

Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Vyombo vya usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Ofisi bora na za kisasa, ununuzi wa vitendea kazi, maslahi ya Askari na upatikanaji wa makazi yaliyo bora.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...