Na Mary Margwe, Simanjiro

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Mirerani Mhandisi Menard Msengi, amesema kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 ofisi yake imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 52 .2 3 ya lengo la makusanyo.

Hayo alibainisha alipokua akitoa taarifa hiyo Kwa Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko,mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dkt.Suleimani Serera, Kamishna wa Madini Abdulyahman Mwanga, Katibu Tawala wa Mkoa huo Caroline Mthapula.

Mhandisi Msengi amesema, jumla ya Makusanyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 ni sh.bil.2,611,657,467.20 ikiwa ni sawa na asilimia 52.23 ya lengo husika.

Aidha alisema eneo la Kitalu C kinaendelea na shughuli zake za uchimbaji ambapo mpaka sasa jumla ya kilograms 146 zimezalishwa zenye thamani ya sh.mil.709,574,190.49 na kuiwezesha Serikali kupata jumla ya sh.mil.49,670,193.33.

Akielezea sababu zilizosababisha baadhi ya malengo kutofikiwa Mhandisi Msengi amesema kuwa ni pamoja na hali ya kijiolojia ya mashapo kuwa katika kina kirefu hivyo migodi mingi kutumia muda mrefu kufanya utanuzi na uwekezaji wa migodi pamoja na ukosefu wa teknolojia za kisasa kwa wachimbaji wadogo ndani ya eneo la ukuta.

Mhandisi Msengi pia amebainisha baadhi ya changamoto zilizopo katika eneo hilo la Mirerani kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za kijamii yaani maji Safi na salama, umeme na ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo ya uchimbaji wa Madini.

Aidha ameeleza mikakati waliojiwekea ni kuongeza vituo vya madini ujenzi kwa ajili ya kupata wadau wengi wanaofanya biashara ya madini ujenzi hasa ya mchanga na kokoto na ufuatiliaji wa karibu wa miradi inayorajiwa kuanzishwa muda si mrefu wa madini ya Kinywe yaliopo karibu la eneo la Mirerani.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopha Ole Sendeka, amempongeza Dkt. Biteko kwa kuleta utulivu kwenye Sekta ya Madini na kumuomba aendelee kuwa balozi katika kuendeleza utulivu kwenye sekta hiyo.

Pia, Ole Sendeka amesema kuwa katika Eneo Tengefu la Mirerani kuna changamoto kubwa ya barabara ya ndani ya ukuta ambayo inasababisha adha kubwa kwa wachimbaji wanao ingia kwenye migodi mbalimbali iliyopo ndani ya ukuta, na pia amemuomba Dkt. Biteko kusaidia upatikanaji wa maji ndani ya ukuta wa Magufuli.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...