Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndg Sophia Mjema ameendelea na ziara yake ya kuvitembelea vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini, ambapo mapema leo tarehe 19 Julai 2023 amelitembelea Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Ndg Mjema amepokelewa na menejimenti ya Shirika hilo ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Ndg Dkt Ayubu Ryoba ambapo amepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za Shirika hilo pamoja na mageuzi makubwa ya TEHAMA ambayo ni jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuliboresha Shirika hilo.

Kwa upande wake kwa niaba ya Shirika hilo na wafanyakazi, Mkurugenzi Mkuu ameshukuru ujio huo wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na kumhakikishia kuwa TBC kama chombo cha habari cha umma kinaendelea kuhakikisha kinasambaa kote nchini ili kuwafikishia Watanzania wote habari za uhakika na kwa wakati.

#CCMIMETIMIA
#KAZIIENDELEE


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...