Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw Hamza Johari amesema kutokana na uhaba wa wataalamu katika sekta ya Anga, Mamlaka hutoa Udhamini wa Masomo ya Anga nje ya nchi ili kuweza kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta hiyo na kuongeza ufanisi.

Bw. Johari aliongea hayo alipofanya ziara kwenye banda la Mamlaka lililopo katika jengo la Karume viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba). Ambapo alisema, kwa mwaka jana Mamlaka iliwadhamini wahandisi 10 kwenda kupata mafunzo ya Matengenezo ya Ndege nchini Ethiopia.

Pia, katika ziara hiyo Bw. Johari alikutana na wadau na kuzungumzia shughuli mbalimbali za kiudhibiti inazozifanya pamoja na huduma mbalimbali za uongozaji ndege inazozitoa.

Pamoja na hayo Mkurugenzi alipata wasaa wa kutembelea mabanda mbalimbali ikiwemo TAA, ATCL, TPA, TRC na ZAA na kujionea shughuli zao za uendeshaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw Hamza Johari  akiwasili kwenye viwanja vya Sabasaba kwa ajili ya kutembea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw Hamza Johari  akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa TCAA alipofika katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw Hamza Johari  akisaini kitabu katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw Hamza Johari  akizungumza na waandishi wa habari alipofika katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...