Na Elias Gamaya, Shinyanga,
MTOTO wa miaka tisa imedaiwa kumuokoa mtoto mwenzake wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa ndani baada ya nyumba yao iliyopo Mtaa wa Mhongolo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kuanza kuteketea kwa moto.
Imedaiwa nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mjane Asha Maziku ambaye alieleza kuwaacha wajukuu zake nyumbani na yeye akiendelea na shughuli zingine za kifamilia.
Akizungumza na mwandishi wa habari nyumbani kwake, Maziku amesema anadhani chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme kwa sababu mashuhuda wamueleza moto ulianzia kuwaka juu ya nyumba na awali hitilifu ilishakwishatokea kwenye nyumba hiyo.
"Ninaishi na wajukuu zangu wanne wawili wanasoma na ndani kulikuwa na watoto hao wadogo, moto ulivyoanza walibebana kutoka nje hakuna aliyefariki bali mali zangu zote zimeteketea ndani, "amesema. Maziku.
Ameongeza kuna watu amesikia walisema ni jiko la gesi limesababisha lakini siyo kweli kwani mtungi wa gesi uliisha miezi sita iliyopita sasa
Kwa upande wake Shakra Mohamed ambaye ni mdogo wake na Asha na jirani amesema moto huo waliona kuanza kuwaka juu ya nyumba saa moja na ilipofika saa tano waliamua kupiga simu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lakini walichelewa kutoka hadi majira ya saa tatu usiku.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo Emanuel Nangale amesema chanzo cha moto hakijafahamik lakini ameshauri wananchi kutowaacha watoto wadogo peke yao ndani ya nyumba." Watoto walionusurika kwenye nyumba hio wamejiokoa wenyewe hiyo ni hatari."
Hata hivyo inaelezwa baadhi ya wananchi wameponda mawe gari la zimamoto na uokoaji lilipokuwa likitokea ofisi za Buzwagi wakifikiria limetoka Manispaa baada ya kuona limechelewa kufika kwa wakati lakini inaelezwa Polisi walifika na kuzuia.
Akizungumzia tukio hilo Mkaguzi kutoka Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama Edward Selemani amesema wananchi walipiga simu na kuelezwa gari ni bovu lakini wao wakafanya jitihada za kuazima gari kutoka Buzwagi.
Ameongeza baada ya kufika wananchi wakaanza kuponda mawe ndipo wakaomba ulinzi wa Jeshi la Polisi ili wazime moto huo usiweze kusambaa kwenye nyumba za jirani.
Home
HABARI
MTOTO MIAKA TISA AMUOKOA MWENZAKE WA MWAKA MMOJA NYUMBA IKITEKETEA KWA MOTO KAHAMA BAADA YA KUACHWA NDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...