Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.


Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Masoko na Mawasiliano Magreth Kageya amesema wanatoa huduma zote ikiwemo kutoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili kwa ajili ya kufanya Mitihani, maelekezo kwa juu ya ulipaji wa ada mbalimbali napia ametoa wito kwa wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA wanaweza kufika katika Banda lao lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya Kihasibu na Kikaguzi.

Pia amesisitiza kuwa Bodi hiyo kwa sasa inatumia mifumo ya kidijitari kutoa huduma zake kwa kupitia tovuti yao.
Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiongozwa na Afisa Masoko na Mawasiliano Magreth Kageya wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda la Bodi hiyo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...