Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi  amesema kwa mara ya kwanza  Maadhimisho ya siku  ya  Mwaka mpya wa Kiislamu;Mwaka 1445  Hijriya kutambuliwa na Serikali kuwa ni siku ya mapumziko.

Serikali imekubali ombi la Waislamu kuhusu kuiadhimisha siku hii na kuwa ya mapumziko kwa madhumuni ya kuipa hadhi na kuiongezea hamasa siku ya mwaka mpya wa Kiislamu kila inapofika.

Ameyasema hayo leo katika hafla ya Maadhimisho  ya kuukaribisha kuingia mwaka mpya wa Kiislamu yaliyofanyika Msikiti wa Munawar Mfikiwa, Wilaya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Kwa Mamlaka ya kikatiba chini ya kifungu  6(1)(a)cha Sheria ya Masuala ya Rais wa Zanzibar,Namba:3 ya 2020, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  ameitangaza rasmi kesho Jumatano itakuwa ni siku ya mapumziko  Kitaifa Zanzibar.

Aidha, Rais  Alhajj Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutimiza wajibu wa malezi ya vijana kuwa na kizazi  chema  chenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa  kutekeleza maarimsho  yake na kujiepusha na makatazo  katika misingi  bora ya maadili kwa mujibu silka na tamaduni za dini. 

Vilevile, kuwa raia wema na wazalendo wa kuijenga nchi  kwa kuendelea kudumisha amani iliyopo kwan kila mmoja.












 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...