NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

RAIS wa Kampuni ya Mafuta ya Shell Tanzania Bw. Jared Kuehl ametembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabsaba Jijini Dar es Salaam.

TPDC wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo mara kwa mara ambapo wanatoa elimu kwa wananchi ambao wanatambelea banda lao ikiwemo kuwaoneha na kuwaelezea miradi mbalimbali inayoendelea kwenye Shirika hilo ikiwemo mradi wa LNG.

TPDC inawakaribisha wadau mbalimbali kuweza kuona na kujifunza Visikuku ambavyo vinasaidia kujua umri wa mwamba na mazingira ambapo mwamba ulitengenezwa baharini au nchi kavu katika uzalishaji wa mafuta na gesi.

Rais wa Kampuni ya Mafuta ya Shell Tanzania Bw. Jared Kuehl akitumia hadubini kutazama visikuku vidogo vidogo vinavyopatikana kwenye miamba wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Julai 6,2023 katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabsaba Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Kampuni ya Mafuta ya Shell Tanzania Bw. Jared Kuehl akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Julai 6,2023 katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabsaba Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...