



Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na mfuko wa Abbott (Abbott Fund) wa nchini Marekani imekubaliana kuimarisha Makao ya kulea watoto mkoa wa Dar es Salaam hasa upande wa maktaba.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya rais wa mfuko huo Melisa Brotz yenye lengo la kujionea maendeleo ya shughuli walizoshirikiana na Serikali kupitia Wizara zilivyotekelezwa hususani makao ya Taifa ya watoto Kikombo jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju ameushukuru mfuko huo kwa ushirikiano na Serikali katika kuboresha miundombinu na hali ya makazi ya taifa ya kulea Watoto.
"Mfuko wa Abbott umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Tanzania, Wizara tumejipanga kuhakikisha inafanikiwa, nawaomba kuendelea kufadhili makao haya ili kupunguza changamoto ya usafirishaji kwa kuwezesha upatikanaji wa Basi pia kuungana na Serikali katika kuwezesha ujenzi wa Makao ya Watoto ya Jijini Dar es salam" amesema Mpanju.
Kwa upande wake Melisa Brotz amesema amefurahishwa na Stadi za kazi, Elimu ya ufundi stadi, Mtindo wa elimu na Maisha wa makao hayo na kuahidi kuwezesha kuongeza miradi na kufadhili ujenzi wa kituo cha ustawi wa jamii cha Dar es salam. Pia kuhakikisha upatikanaji wa vitabu vya Kiingereza na Kiswahili kwa maktaba ya makao ya kukea watoto jijini Dar es salaam.
Makao ya Taifa ya kulea Watoto Kikombo ni mpango wa kusaidia programu za watoto wanaoishi katika mazingira magumu Tanzania Bara kwa ushirikiano na mfuko wa Abbott. Makao hayo yana maeneo ya shamba, karakana, hosteli za Watoto, madarasa na makataba, ambayo mfuko umekua ukiyaimarisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...