Na.VERO IGNATUS ARUSHA

Serikali imesema kwa kipindi cha miaka mitano Iliyopita Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya shilingi bilioni 79 kwaajili ya sekta ya elimu ambapo kiasi cha shilingi bilioni 25 ni kwaajili ya miundombinu ya miradi ya elimu, shilingi bilioni 54 kwaajili ya elimu bila malipo.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari julai 8 Jijini Arusha na kwamba katika kipindi hicho jumla ya vyumba vya madarasa 810 yenye thamani ya bilion 16.2 vimejengwa na kufanya mkoa katika shule za sekondari kuwa na jumla ya madarasa 3,093

Akizungumzia kuhusu abiria wanaoingia nchini Msigwa amesema kwa rekodi za 2022/23 KIA imeweza kuhudumia zaidi ya abiria 900,000 ambapo kwa mwaka 2019/20 uwanja ulihudumia abiria 720,000 hiyo ni kwa mujibu wa tafiti zinazofanyika ambapo abiria wanaoshuka katika uwanja wa kimataifa wa kia kwa 60%ni watalii

Aidha serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na wadau kwa kujenga uwanja wa KIA ambao unafanya vizuri, kwani kwa sasa kuna ndege;10 za kimataifa zinazotua katika uwanja huo

Amesema katika mkoa wa Arusha yapo majengo ya kisasa 4 kwaajili ya huduma za dharura EMD katika hospitali ya rufaa ya Mountmeru Karatu, Ngorongoro sambamba na wodi mbili za wagonjwa mahutihuti (ICU)Mountmeru na Longido.

Aidha mkoa wa Arusha una huduma ya dharura wa mika mitano iliyopita serikai imeongeza huduma za kutolea matibabu kitoka 383 hadi kufikia vituo 42 halmashauri zote saba za mkoa zina hospitali zenye hadhi ya wilaya.

"Serikali imeweza kukarabati vituo vya Afya 25 zahanati 45 na vyumba vya watumishi 26 katika mkoa wa Arusha "Alisema

Msigwa alitoa ufafanuzi juu ya ndege ya Airbus 220 iliyoliyokuwa imeshikiliwa nchini Uholanzi iliyokuwa chini ya sheria tayari serikali imeshafanya mazungumzo julai 7tayari ndege hiyo imerudi nchi.

Akizungumza kuhusu ujazaji maji katika Bwawa la umeme la Julius Nyerere la mto Rufiji amesema kuwa inaendelea kwa kiwango kilichopangwa cha kufikia mita 163 juu ya usawa wa bahari ambapo tayari maji yameshafikia januari 2024 inawezekana ujazo wa maji ukafikia ujazo wa mita 184 ambapo majaribio yanatarajiwa kuanza februari 2024 na mwezi juni uzalishaji rasmi utaanza.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...