Kamati ya Olimpiki Tanzania itaadhimisha Siku ya Olimpiki kitaifa hapo tarehe 08/07/2023, kuanzia saa 12.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Lets Move" kauli ambayo inadhamiria kuhamasisha kila mtu kufanya mazoezi kwa ajili ya afya na kuuweka mwili sawa.

Sherehe hiyo itahusisha mbio za taratibu za kilomita 2.5 kwa Watoto chini ya miaka 14 na kilomita 5.0 kwa walio na miaka 15 na kuendelea. Pia itahusisha halaiki yamazoezi (aerobics), breakdance" na mpira wa mezani (Teqball).

Siku ya Olimpiki husherehekewa kila mwaka tarehe 23 Juni, ikiwa kumbukumbu yakuanzishwa kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa hapo tarehe 23 Juni, 1894, Paris nchini Ufaransa.

Imetolewa na Filbert Bayi,

KATIBUMKUU - KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

 Kwa mawasiliano zaidi +255 754 28717 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...