Na Philipo Hassan, Kilimanjaro

Mwanamziki na mpiga kinubi maarufu Duniani Prof. Siobhan Brady kutoka nchini Ireland mwenye rekodi ya Guinness  akiwa na timu yake wamewasili katika Lango la Machame kwa ajili ya kutimiza azma yake ya kuvunja rekodi ya  dunia kupiga kinubi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro  ambacho ni kilele kirefu kuliko vyote barani Afrika chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza katika hafla ya kumuaga Siobhan na timu yake kwenda kufanya tamasha la kupiga kinubi kileleni, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas amempongeza Siobhan na timu yake ya Highest Harp Concert kwa kuja kuvunja rekodi katika kilele cha Mlima huo na kumtaka awe balozi mzuri atakaporudi nchini Ireland na hata kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii autangaze na kuusemea vizuri ili kuvuta watalii wengi zaidi kupanda Mlima Kilimanjaro.

Dkt. Abbas aliendelea kwa kueleza kuwa haya ni matunda ya Filamu The Royal Tour aliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  aliyekuwa "Guide" namba moja kunadi vivutio vinavyopatikana Tanzania katika masoko ya Kimataifa.

Aidha, Dkt. Abbas pia aliyataka Makampuni ya Utalii yatoe taarifa kuhusu wageni Mashuhuri wanaokuja kutembelea Tanzania ili tuendelea kujitangaza kimkakati kupitia ziara zao, kuwahudumia vizuri na kuwajengea mazingira mazuri yatakayowawezesha kuwa mabalozi wazuri wa  kuisemea Tanzania katika uga wa utalii.

Naye, Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Mary Oniel ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwapokea na kuwakarimu vizuri wageni hao. Pia alieleza kuwa ujio wa mpiga kinubi huyo utasaidia kuongeza watalii wengi kutoka taifa la Ireland kutembelea Tanzania.

Siobhan Brady ameianza safari ya kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro  kupitia Lango la Machame leo tarehe 20.07.2023 kuhitimisha ndoto yake.
Ikumbukwe kuwa mwanadada huyo alishavunja rekodi ya Guinness Book of World Records (GWR) mwaka 2018 katika Milima ya Himalaya (Singla Pass) India wenye urefu wa futi 16,000ft.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...