NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa huduma kwa wajasiriamali ,wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Viwango katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo wamekuwa wakiwapa taarifa ya huduma ambazo wanazitoa ikiwemo uandaaji wa viwango,usajili wa bidhaa na majengo ya vyakula na vipodozi,upimaji,ugezi,uthibitishaji wa mifumo na udhibiti ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 10,2023 Jijini Dar es Salaam, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi Bw.Hassan Juma amesema wameweza kupata wadau mbalimbali wakiwemo wajasirimali wadogo ambao wameweza kupata elimu namna ya bidhaa zao zinavyotakiwa kuthibitishwa ubora na Shirika hilo kupitia SIDO.

"Kwenye Maonesho ya kipindi hiki wajasiriamali wengi wameonesha nia ya kuthibitisha bidhaa zao baada ya kupata elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kuthibitisha bidhaa zao ambazo wamekuwa wakizizalisha pamoja na kuagiza". Amesema

Pamoja na hayo Bw.Juma amesema kuwa kupitia Maonesho hayo wameweza kutoa elimu kwa makampuni makubwa mbalimbali kuhusiana na uthibitishaji wa mifumo yao ambao wameridhishwa na huduma zinazotolewa na shirika hilo.

TBS inaendelea kuwakaribisha wadau kutembelea banda lao lililopo kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ili kupata huduma hizo papo kwa hapo.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...