Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
WANAFUNZI zaidi 700 katika Shule ya Msingi Kikelelwa wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamejengewa matundu ya vyoo 18 na Benki ya Taifa ya Kibiashara (TCB) na hivyo kuwaepusha wanafunzi hao kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na uchakavu wa vyoo walivyokuwa wanatumia awali.
Akizundua vyoo hivyo shuleni hapo Mkurugenzi wa Hazina Tanzania Commacial Bank Wenceslaus Fungamtama kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kujenga vyoo hivyo ni kuboresha mazingira na utulivu wa kujifunza kwa wanafunzi hao wawapo shuleni.
"Ili kuunga jitihada za Serikali za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu TCB tumekuwa tukitenga zaidi ya Sh.milioni 300 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimeweza kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika maeneo mbali hapa nchini" amesema Fungamtama.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Charles Amos amesema kutokana na uchache wa matundu ya vyoo yaliyokuwepo awali wanafunzi walilazimika kupanga foleni ya kusubiriana huku wale wadogo kujikojolea.
"Tunawatoto waliokuwa wanatoroka kwenda nyumbana kwa aibu ya kujikojolea, hasa muda wa mapumziko ambao wanatoka darasani kwa pamoja, lakini sasa kwa vyoo hivi ni wazi kutakuwa na utulivu wa kujifunza" amefafanua Mwalimu Amos
Awali Dada mkuu wa shule hiyo Careen Jonas ameonyesha furaha yake kuwa licha ya vyoo hivyo kujengwa kisasa, vikizingatia miundombinu ya walemavu, pia vina chumba maalumu cha kubadilishia nguo kwa waschana wawapo kwenye siku zao za hedhi.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Alice Makule amesema kwa sasa shule inajumla ya wanafunzi 768, wavulana 385 na waschana 378.
"Ambapo kwa uwiano ilitakiwa kuwe na matundu 16 kwa wavulana na 19 kwa waschana lakini wakitumia matano matano tu hivyo ujio wa benki hiyo kujenga matundu 18 umepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa."
Shule ya msingi Kikelerwa ambayo ipo mpakani mwa Tanzania ni moja kati ya shule kongwe za mkoa wa Kilimanjaro, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uchakavu wa madara, vyoo na uchache wa walimu lakini imeelezwa kufanya vizuri kiufaulu.
Mkurugenzi wa Hazina Wenceslaus Fungamtama, wa pili kulia ni Ofisa Elimu idara ya elimu msingi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Alice Makule na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Charles Amos wakishiriki kukata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa matundu ya vyoo 18 yaliyojengwa na TCB
Mkurugenzi wa Hazina akikagua Matundu ya vyoo baada ya kukata utepe akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chichi Banda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...