NA PAUL WILLIUM, MOSHI.
UPELELEZI katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikiwakabili waliokuwa wafanyakazi watatu wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro(KCBL) umekamilika huku upande wa mashitaka ukiwasilisha mahakamani mashahidi 29 na vielelezo vipatavyo 471.
Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2023 ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Salome Mshasha huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Mawakili wa serikali Donasian Chuwa, Samwel Kaaya, Henry Kasiano Daudi na Bora Msafiri Mfinanga.
Itakumbukwa kuwa mnamo Octoba 2019, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro iliwafikisha katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Joseph Kingazi, na Elizabeth Makwabe wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi na baadaye Juni, 2021 aliyekuwa mhasibu wa benki hiyo, Ombeni Masaidi aliunganishwa katika kesi hiyo.
Washitakiwa hao kwa pamoja walikuwa wanashitakiwa kwa makosa 13, ikiwemo makosa 9 ya kughushi na kutoa nyaraka za uongo, kosa moja la kuongoza uhalifu wa kupanga, kosa moja la ubadhirifu wa fedha za umma na kuisababishia mamlaka hasara ya zaidi ya Sh2.4 bilioni.
Home
Unlabelled
UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOWAKABILI WALIOKUWA WATUMISHI BENKI YA USHIRIKA KCBL WAKAMILIKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...