Na Abdullatif Yunus - Michuzi Blog Kagera
Taasisi ya fedha inayojihusisha na kuweka Akiba na Kukopa ya Umoja wa Vijana Karagwe SACCOS LIMITED UVIKASA imekabidhi Pikipiki 37 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 85 kwa Vijana wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa ikiwa ni sehemu ya Mkopo kwa Vijana hao ili ziwawezeshe kuwainua Kiuchumi.
Hafla ya kukabidhiwa Pikipiki hizo imefanyika Mnamo Julai 10, 2023 katika Viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilayani Karagwe Mjini Kayanga, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo wanachama wa Saccos.
Awali akiongea katika Hafla ya KUkabidhi Pikipiki hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya UVIKASA Yahya Kateme ambaye pia ni muasisi wa Saccos hii, amesema kuwa pikipiki 37 zilizotolewa ni aina ya SANYA CC 150 zenye thamani ya shilingi milioni 85 na kusema kuwa licha ya Mkopo huo bado kuna changamoto ya Wanachama kutorejesha kwa wakati marejesho ya pikipiki hizo ambazo hutolewa kwa mkataba, na kuongeza kuwa mpaka sasa Kiasi cha Madeni zaidi ya Shilingi Milioni 900 zinadaiwa ikiwemo pesa Taslimu.
Naye mgeni Rasmi katika hafla hiyo Ndg. Anatory Nshange Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Karagwe amesema kuwa suala la Vijana ambao hawajarejesha mikopo litashughulikiwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Karagwe kwani ambao hawarejeshi wanakwamisha vijana wenzao kukosa fursa ya kukopa.
Mbali na Mikopo hiyo waliopewa, pia Wanachama hao wameunganishwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ikiwa lengo ni kuwazoesha Vijana hao kuwa na utaratibu wa kuweka Akiba itakayowafaa baadae, na Komredi Kateme akithibitisha hilo kwa kuwalipia Mchango wa kwanza wa Shilingi Elfu Ishirini kila mmoja.
Aidha kwa upande wake Sajenti Mafulu Kahitila kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya Karagwe Awali akitoa Mada juu ya Sheria za uendeshaji Vyombo vya Moto, amesema kuwa Vijana waliokabidhiwa Pikipiki hizo wanao wajibu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kuongeza kuwa baadhi ya waendesha Pikipiki hasa kundi la vijana wamekuwa hawazingatii sheria za Usalama Barabarani hali inayosababisha baadhi ya Vijana kupata Vilema na wengine kufariki kabisa.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Kukabidhi Pikipiki Ndg. Anatory Nshange akikabidhi Kadi za Wanachama wapya wa NSSF ambao ni Vijana wa UVIKASA mara baada ya kuunganishwa na Mfuko huo wa hifadhi ya Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya UVIKASA LTD Ndg. Yahya Kateme ambaye ni Muasisi wa SACCOS hiyo akitoa Salaam zake wakati wa Hafla ya Kukabidhi pikipiki hizo.
Mgeni Rasmi Ndg. Anatory Nshange Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Karagwe akihutubia Wanachama na wageni wakati wa Hafla ya Kukabidhi Pikipiki 37 kwa Wanachama wa UVIKASA
Sehemu ya Vijana wa UVIKASA ambao ni wanufaika wa Mikopo hiyo wakiwa katika Hafla ya kukabidhiwa Pikipiki zao.
Wafanyakazi wa UVIKASA wakiwa na Baadhi ya Wanufaika wa Mikopo ya Pikipiki mara baada ya kukabidhidhiwa Pikipiki zao
Picha ya Pamoja Meza Kuu na Wafanyakazi Picha ya Pamoja Meza Kuu na Wafanyakazi wa UVIKASA LTDwa UVIKASA LTD
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...