Njombe
Wizara ya afya imetoa onyo kwa watumishi wa afya nchini watakaobainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa dawa na vitendanishi kwenye vituo vya kutoa huduma za afya na kuwataka watumishi kuwa waaminifu ili kuepuka hatua wanazoweza kuchukuliwa ikiwemo kufutiwa usajili na kupelekwa Mahakamani.
Onyo hilo limetolewa na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt,Grace Magembe wakati akizungumza na watumishi wa wizara hiyo walipofika na kukagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe iliyopo Wikichi mjini Njombe.
"Kwenye sekta ya afya tunapewa Bilioni 20 kila mwezi,hizo dawa sio za kwetu ni kwa ajili ya wagonjwa wanaokuja kwenye vituo vyetu lazima zitumike kwa usahihi hakutakiwi kuwe na ubadhilifu,wizi wa dawa vitendanishi sijui kitu gani na ni waambie kwenye hilo tukikugundua unashiriki kuiba dawa,kuziuaza hatutakuacha salama"alisema Dkt,Magembe
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Juma Mfanga ameishukuru serikali kwa kutoa watumishi 159 ndani ya mkoa huo ili kuendelea kuboresha hali ya utoaji wa huduma.
"Tunaishukuru serikali tumepata watumishi 159 na kati ya hao wote wamesharipoti ni watumishi 6 tu ambao hawajaripoti na tumeshatoa taarifa kwa mamlaka husika"Amesema Mfanga
Dkt,Wilfred Kiambile ni mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe amesema hosptali hiyo imeendelea kufanikiwa kwa kiasi kikubwa huku pia ikiongezewa madaktari bingwa pamoja na kuongezeka kwa huduma za pimaji hatua iliyosababisha kupungua kwa rufaa kwenda hospitali za kanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...