Na. Damian Kunambi, Njombe.
Waziri wa Utamaduni, sanaa na michezo Balozi Dkt. Pindi Chana, ameviasa vikundi mbalimbali vya sanaa hapa nchini kujisajili katika Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ili viweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo.
Waziri Chana ameyasema hayo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Madilu iliyopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa lengo la kukabidhi msaada wa bati 152 zenye thamani ya zaidi ya sh. Mil 5.
"Mkijisajili mtaweza kutambulika na mtafungua milango ya fursa mbalimbali kama kupatiwa mikopo, kupata mialiko ndani na nje ya nchi pamoja na fursa nyingine nyingi ambazo hamkuwahi kuzipata hivyo fikeni kwa maafisa utamaduni waliopo katika halmashauri zenu muweze kupatiwa utaratibu" Amesems Dkt. Pindi Chana.
Sanjari na hilo pia ameziagiza halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha zinatenga maeneo kwaajili ya viwanja vya michezo mashuleni ili wanafunzi waweza kukuza vipaji sambamba na kujenga afya zao.
Amesema wanafunzi wawapo mashuleni wanapaswa kushiriki michezo mbalimbali ambapo katika kusapoti hilo aliwakabidhi mipira miwili wanafunzi wa shule ya Madilu ambapo mmoja kwaajili ya wanafunzi wa kiume na mwingine kwa wanafunzi wa kike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...