NA STEPHANO MANGO, SONGEA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama ameanza ziara ya kikazi katika Jimbo la Peramiho ya kukagua miradi inayotekelezwa Jimboni humo,kuzungumza na wananchi, na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi na Serikali

Akizungumza katika ziara hiyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Waziri Mhagama alisema kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Peramiho wanaendelea kumshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza uchumi kwa Wananchi hususani wakulima kwa kuwasongezea huduma za ruzuku karibu na maeneo yao na kwa bei nafuu, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa ya kilimo vizuri ili kukuza uchumi.

“Pamoja kuwa mnajishughulisha na shughuli za kilimo pia endeleeni kubuni vyanzo vingine vya kuingiza mapato kwani Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la maendeleo ya wananchi imejipanga vizuri ili kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora na salama”, amesisitiza Waziri Mhagama

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama ameweka Jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Muungano , ambapo madarasa hayo yalianza kujengwa kwa nguvu za wananchi ambapo Halmashauri ilipeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 29.6 kutoka mapato ya ndani na milioni 2.5 kutoka mfuko wa Jimbo kwa ajili ya ukamilishaji.

Aidha katika ziara hiyo amegawa vifaa tiba mbalimbali katika Zahanati ya Namatuhi vikiwemo viti vya kutembelea wagonjwa 6 ambapo viti 3 kati ya hivyo wamekabidhiwa wagonjwa, shuka, drip stand, taulo za kike, blanketi na vyandarua vya kujikinga dhidi ya Malaria kwa Wazee.

Aidha, Jenista amewataka Wananchi kuacha tabia za kukata miti ovyo katika maeneo yao na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji kwani huo ni uharibifu wa mazingira unaosababisha kukosekana kwa maji.

Vilevile Waziri Mhagama amewaasa vijana kutojishughulisha na shughuli za kilimo cha bangi na matumizi ya madawa ya kulevya kwani inaleta athari kubwa katika Afya ya akili.

Ziara hiyo imeanza Julai 9, mwaka huu ambapo ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwalimu Neema Maghembe, Viongozi wa Chama, Madiwani pamoja na timu ya Wataalamu






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...