Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Young Africans SC rasmi imekabidhiwa kiasi cha fedha shilingi Milioni 405 (Tsh. 405,000,000) kutoka Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportpesa baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC).

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Sportpesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema wanajivunia kuendelea kuwa wadhamini wakuu wa Klabu hiyo yanye mafanikio na uongozi imara.

“Mafanikio wanayoyapata Young Africans SC yanakuja kutokana na kufanya kazi kwa uweledi na kuendesha Klabu hii kisasa,” amesema Tarimba.

Kwa upande wake, Rais wa Yanga SC, Mhandisi Hersi Said amesema wanajivunia kwa mafanikio waliyoyapa msimu uliopita na wamewashukuru Sportpesa kutambua jitihada hizo walizofanya za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho (ASFC).

“Tunashukuru kupata kiasi hiki cha fedha kutoka kwenu Sportpesa, tunaamini kiasi hichi ni chachu kwetu kufanya vizuri msimu mwengine wa mashindano, tunaamini tutafanya vizuri zaidi,” amesema Mhandisi Hersi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...