TAASISI ya Afya Check kwa
kushirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga wanatarajia kuzindua
kambi maalum ya kupima afya bure kwa wananchi wa Jiji la Tanga kwa
siku tano ikiwa ni mpango wa kuihamasisha jamii kuwa na desturi ya
kupima afya zao mara kwa mara ili pale wanapogundulika kuwa na matatizo
mbalimbali waweze kupata matibabu ya haraka.
Akizungumza na
waandishi wa Habari leo Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Tanga Ummy Mwalimu amesema kambi hiyo itafanyika kwa muda wa siku tano
kuanzia Augost 21 ambapo wananchi 5000 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi
katika magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu, Saratani ya tezi
dume,saratani ya mlango wa kizazi.
Waziri Ummy amesema
magonjwa yatayopimwa ni yale yanayoambukiza na yasiyoambukizwa na endapo
mtu atakutwa na ugonjwa atapatiwa tiba bure na kwa wale ambao watakuwa
na magonjwa yatakayohitaji upasuaji watapatiwa tiba watakapokuja
madaktari bingwa huku akiipongeza banki ya CRDB ambao ndio wadhamini
wakuu wa kambi hiyo.
"Takwimu inaonesha wapo watu laki mbili
ambao hawajajitambua afya zao katika upimaji wa vvu, tunawashauri na
kuwahamasisha watu kupima na kama watu wote ambao wana maambukizi
wangekuwa wanafuata masharti ya kumeza dawa tunaweza kuutokomeza kabisa"
amesema.
"Niwapongeze sana sana wadau wetu wakubwa CRDB,
benki yetu kwa kujitolea na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufadhili huduma
zinazowasaidia wananchi" amebainisha.
"Sasa, nitoe wito kwa
wananchi wote wa Mkoa wa Tanga kujitokeza, wilaya zote kujitokeza kuja
kupima katika viwanja vya shule ya sekondari ya Usagara, lengo ni watu
5000 lakini hata tukipata zaidi itakuwa vizuri" amesisitiza.
Awali
akizungumza Mratibu mkuu wa Afya check Isack Maro amesema lengo la
kuweka kambi mkoani hapa ni kutaka kuwajengea wananchi tabia ya kupima
afya kwa hiyari mara kwa mara na hii ni mara baada ya kumaliza mkoani
Dar es salaam ambapo zaidi ya wananchi 9324 walifanyiwa vipimo.
"Kitakwimu
watanzania tunatumia gharama kubwa sana kujitibu na mara nyingi ni kwa
sababu tumechelewa kugundua tatizo sasa kampeni hizi zilianzishwa
kuhakikisha kwamba watanzania wanajenga tabia ya kuoenda kupima afya
zao mara kwa mara na hii inaonyesha kuyokana na matukio tunayoyaona
kutokana na hizi kambi ambazo tumezifanya kwa muda mrefu"
"Kwa
sasa hivi ndio tumetoka kumaliza vipimo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es
salaam na wilaya zake zote na tukafanikiwa kuwapatia huduma za afya za
bure wananchi takriban 9324 walifanikiwa kupatiwa huduma zote za
kibingwa pamoja na hufuma za kawaida bila kusahau wakapatiwa dawa na
vipimo"
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema leo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati wa mkutano huoMstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...