Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MSEMAJI wa Klabu ya soka ya Yanga Ally Kamwe amejigamba kuwa hakuna tajiri yoyote mwenye uwezo wa kuibomoa timu hiyo huku akitoa siri ukitaka kuibomoa basi inabidi umsajili Rais wa Klabu hiyo Injinia Hers ambaye ndiye anafanya usajili wa wachezaji wanaojua kusakata kabumbu.

Ameyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea mchezo wa marudiano wa michuano ya Klabu Bingwa hatua ya Makundi ambapo watacheza na Asas Djidbouti katika Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salamaa Jumamosi ya wiki hii.

Amesema timu ya Yanga katika upande wa wachezaji iko vizuri na kwa sasa Yanga sio kauka nikuvae."Hatuko  hivyo,  tumeshavuka huko,  tukikwambia panga kikosi cha Yanga hutaweza.Kama kuna mtu anataka kuibomoa Yanga aje kumsajili Injinia Hers."

Kutokana na ubora wa kikosi chao amewapiga kijembe wale ambao wanataka kuibomoa timu hiyo wakawaambie hao Warab waje wamsajili Injinia Hers lakini akibakia  Injiania anachukua mchezaji chuma na wakati huo huo akitokea anayehitaji kumsajili mchezaji wa Yanga  hawaachi hela.

Kuhusu mchezaji wao Scudu Makudubele amesema alienda kwao Afrika Kusini kwa ajili ya kupata hati ya kusafiria baada ya aliyonayo kuonekana imejaa, hivyo aliona atumie muda huu kwenda kwao na kesho anarejea nchini.

"Scudu kweli alienda Afrika Kusini na Jumamosi atakuwepo uwanjani , lakini kocha mkuu Gamond ndio ataamua acheze au asicheze.Alienda kushughulikia pasoport yake,  kesho ataingia nchini, kama ambavyo mlienda kumshuti kinyemela na kesho waende wamshuti vizuri anarudi.Waandishi watapewa ratiba ya muda."

Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba uongozi wa Yanga haumpangii Kocha Gamond nani acheze na nani asicheze,  kwani hilo liko kwenye maamuzi yake na wala hapangiwi.

"Gift Fred yupo lakini haonekani kwasababu ya upangaji tu,  ndio maana jana Lomalisa jana hajaonekana uwanjani.Wachezaji wanacheza kwa zamu lakini  ukuta haujaguswa.

"Hivyo Gift yupo na atapata nafasi yake,  kibwana pia hamjamuona, hajapata nafasi yake.Yanga tulichukua  wachezaji, hatujakusanya wachezaji kujaza idadi," amesema Ally Kamwe.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...