BARAZA la Wazee Wilaya ya Same mkoani kilimanjaro limetoa shukrani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo.

Aidha baraza hilo limempongeza pia Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kaslida Mgeni kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kwa wananchi wa wilaya hiyo

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Same Thimos Mgonja amesema Rais Samia amewapatia tunu kwenye Wilaya hiyo ya Same kwa kuwapatia kiongozi shupavu, jasiri na msimamizi katika kuweka usawa wa kila mwananchi.

"Hivyo basi kama baraza hatuna buti kumpongeza Mkuu wa wilaya Same na tutaendelea kumpatia ushirikiano wa kutosha hasa katika kuleta maendeleo ya wilaya yetu.

"Lakini kwa kipekee tunaunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuijenga nchi yetu na kama Taifa tumepata kiongozi muajibikaji kweli kweli, " amesema.

Ametumia nafasi hiyo kumuomba Mkuu wa Wilaya ya Same kufikisha salaam zao kwa Rais Samia na wanamuombea mema na asikubali kukatishwa tamaa na watu wachache.

"Kama wazee wa wilaya hii tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha atutomuangusha kwani ni kiongozi makini sana katufanyia mengi wananchi wa wilaya ya Same na Taifa kwa ujumla."

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Same Kaslida Mgeni amewashukuru wazee kwa pongezi hizo na kuhaidi kufikisha salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Hassani.

Pia amewahasa wazee kukemea vitendo vibaya kwa vijana wao ambavyo siyo maadili yetu Watanzania kama ulimaji na utumiaji wa zao la mirungi na bangi kwani wanapoteza nguvu ya Taifa hasa kwenye wilaya hiyo.

Amewaomba wazee hao kuwahamasisha vijana kulima mazao ya kawaida hasa zao la mkonge ni zao nzuri na lenye manufa mkubwa

"Lengo langu ni kuhakikisha wananchi Same wanapata maendeleo kupitia kilimo cha mkonge na mazao mengine maparachichi kufanya kazi kwa bidii hili tuendelee kukuza uchumi wa wilaya yetu na Taifa kwa ujumla."







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...