Na Mwandishi Wetu


Benki ya Exim kupitia programu yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) inayojulikana kama “Exim Cares” imezindua Programu ya Uwezeshaji Wanawake (WEP) inayolenga kukuza maendeleo ya kiuchumi katika nchi ambazo benki hiyo inafanya kazi zake zikiwemo Tanzania, Comoro, Djibouti na Uganda.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na mahafali ya kwanza ya program hiyo ambapo wahitimu 20 kwa awamu ya kwanza walikabidhiwa vyeti huku waliefanya vizuri wakipewa zawadi za fedha kama motisha

Programu ya benki sura ya incubator' ambapo makampuni yanayomilikiwa na wanawake na/au wajasiriamali binafsi watasaidiwa kuendeleza biashara zao na kupata huduma mbalimbali zikiwemo mafunzo, mitaji ya kuanzia na rasilimali za kifedha ili kuanza au kuendeleza biashara zao.

Kwa Tanzania, programu ya benki hiyo inawiana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 na itakuwa chachu katika kuimarisha ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa wanawake.

Akizungumza katika uzinduzi wa program hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu jana, benki alisema benki yake imejipanga kuongeza muunganisho wa uendelevu katika mifumo na mbinu zake za kibiashara ili kuleta manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa wadau wake wote.

Matundu alisema program hiyo ya WEP itaendeshwa kwa miaka 5 na itakuwa na athari chanya na kunufaisha zaidi ya wanawake laki sita ifikapo mwaka 2028.

“Programu yetu mpya itahusisha kwa karibu uhamasishaji wa upatikanaji wa fursa hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi nchini,” Matundu alisema.

Alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi nyingine barani Afrika na kuongeza kuwa kuwajengea uwezo kutachangia pakubwa katika kukuza uchumi na kuboresha maisha kwa watu na familia.

"Kama benki, tunaamini kuwa kusaidia wanawake kwa muda mrefu kunakuza maendeleo ya kiuchumi. Kukuza maendeleo ya uchumi jumuishi bado ni kipaumbele kwetu." Alisema.

Matundu aliongeza kuwa uwezeshaji wa wanawake na ujasiriamali unasalia kuwa nguzo muhimu za mipango ya maendeleo barani Afrika na kuongeza kuwa hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanawake ambao wanashika nafasi za uongozi katika sekta za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

"Tafsiri ya hili katika uwezeshaji wa jumla wa wanawake bado inakosekana kwa kiasi fulani kwa sababu mipango na sera zinazohusika za kuwapandisha wanawake kwenye nafasi za maamuzi mara chache haziangazii au kubadilisha masuala ya kimsingi na ya kimfumo ambayo yalisababisha pengo kati ya mamlaka rasmi na halisi ya wanawake; "alisisitiza.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati uzinduzhi huo ailiishukuru Benki ya Exim kwa kuanzisha programu hiyo huku alkisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kuwainua wanawake kwa kuanzisha jitihada mbalimbali zikiwemo kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ambao unatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuwawezesha wanawake.

“Kwa jitihada hizi endelevu zinazofanwa na benki ya Exim, kakika mmetuheshimisha sana na sisi kama Serikali tunawaahidi hatutawaangusha,” alisema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajia alisema kuwa pamoja na mafanikio yanayoendelea kupatikana kwenye maeneo mengine kijinsia, kwa sasa changamoto kubwa bado imebaki kuwa, wanawake wengi bado hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira.

“Kwa takwimu nilizonazo, takriban asilimia 70 ya wanawake bado wapo kwenye ajira zisizo rasmi wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama mama ntilie na kazi za majumbani, n.k,” alisea

Alisemsa kwa mujibu wa takwimu za Finscope za mwaka 2017, kati ya watu 3,014,106 waliokuwa kwenye ajira rasmi, wanawake walikuwa 1,107,917 sawa na asilimia 36.8 tu.

“Na kwa mujibu wa utafiti wa Finscope 2023 ambao umetoka miezi michache iliyopita, pengo la jinsia la ujumuishaji wa kifedha limepungua kutoka asilimia 10-pointi mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 3-pointi mwaka 2023,” aliongeza.

Aliseme hata hivyo, pengo la jinsia kwa sekta ya kibenki lilibakia sawa, na takriban asilimia 9 -point ya wanaume zaidi kupata huduma za benki ukilinganishwa na wanawake.

“Hii inaendelea kudhihirisha kutokuwepo na uwiano sawa wa huduma za kifedha kati ya wanawake na wanaume.Ni matumaini yangu kuwa programu hii ya WEP ya Benki ya Exim imekuja muda muafaka na itakuwa chachu ya kupunguza pengo hili na kuwafanya wanawake washiriki kikamilifu katika sekta ya kifedha,” alisema.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima (wa pili kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Programu ya Uwezeshaji Wanawake (WEP) ya Benki ya Exim katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima (wa pili kulia) ajifurajia jambo wakati wa uzinduzi wa Programu ya Uwezeshaji Wanawake (WEP) ya Benki ya Exim katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu. Na Mpiga Picha Wetu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...